TANGAZO


Sunday, September 22, 2013

Redd's Miss Tanzania alivyopatikana ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam

Wapenzi waliohudhuria katika shindano la kumsaka Redd's Miss Tanzania 2013, wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakitendeka wakati wa shindano hio. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya washiriki wa shindano hilo wakiwa wamevalia magauni ya kutokea.
Baadhi ya washiriki wa shindano hilo wakiwa wamevalia magauni ya kutokea.
Baadhi ya washiriki wa shindano hilo wakiwa wamepozi na magauni ya kutokea.
Washiriki wa shindano hilo wakiwa wamepozi mbele ya mashabiki na wadau wa urembo ukumbini humo.
Mshindi wa Redd's Miss Tanzania 2013, Happines Watimanywa akionesha vazi lake la ufukweni wakati wa shindano hilo.
Mshindi wa Redd's Miss Tanzania 2013, Happines Watimanywa (kushoto), akiwa na mshiriki mwenzake, Neema punga mkono huku akiwa na mshindi wa Pili,  Latifa Mohamedi (kushoto) na wa Tatu, Clara Bayo, mara baada ya kuvishwa taji hilo, ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam juzi usiku.  

Baadhi ya washiriki wakiwa katika shindano hilo ukumbini humo.
Baadhi ya warembo wa kinyang'anyiro hicho wakiwa wamepozi wakati wa shindano hilo.
Warembo walioingia katika 15 Bora wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa shindano hilo.
Warembo waliokuwa wameingia moja kwa moja kwenye 15 Bora wakiwa na maua yao baada ya kujishindia nafasi za kwanza katika mashindano ya Photojenic, Modling nk.
Jaji Mkuu wa shindano hilo, Ramesh Shah, akitaja 5 Bora mbele ya washiriki walioingia kwenye 15 Bora wa Redd's Miss Tanzania 2013.

Washiriki walioingia kwenye 15 Bora wa Redd's Miss Tanzania 2013, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa kuingia katika hatua hiyo.
Warembo walioingia kwenye 5 Bora wakiwa tayari kwa hatua ya mwisho ya kujibu maswali ya majaji wa shindano hilo.
Washiriki walioingia Tano Bora wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa.
Happines Watimanywa akijibu swali aliloulizwa na majaji wakati wa kumtafuta mshindi wa shindano hilo, akiwa na wenzake walioingia katika Tano Bora ya shindano hilo.
Baadhi ya majaji wa shindano hilo wakifurahia jambo wakati wa shindano hilo.

Mshindi wa Redd's Miss Tanzania 2013, Happines Watimanywa akiwapungia mkono mashabiki waliokuwa wamefurika kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.  
Mshindi wa Redd's Miss Tanzania 2013, Happines Watimanywa (katikati), akipunga mkono huku akiwa na mshindi wa Pili,  Latifa Mohamedi (kushoto) na wa Tatu, Clara Bayo, mara baada ya kuvishwa taji hilo, ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.  
Mshindi wa Redd's Miss Tanzania 2013, Happines Watimanywa (katikati), akipunga mkono huku akiwa na mshindi wa Pili,  Latifa Mohamedi (kushoto) na wa Tatu, Clara Bayo, mara baada ya kuvishwa taji hilo, ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mshindi wa Redd's Miss Tanzania 2013, Happines Watimanywa akipunga mkono mara baada ya kuvishwa taji hilo, ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.  
Mshindi wa Redd's Miss Tanzania 2013, Happines Watimanywa akipunga mkono mara baada ya kukabidhiwa gari lake, ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.  
Mshindi wa Redd's Miss Tanzania 2013, Happines Watimanywa akikabidhiwa funguo za gari lake hilo.  
Mshindi wa Redd's Miss Tanzania 2013, Happines Watimanywa akionesha funguo za gari lake hilo.
Mshindi wa Redd's Miss Tanzania 2013, Happines Watimanywa akipongezwa na Meneja wa kinywaji cha Redd's, Victoria Kimaro, wadhamini wakuu wa shindano hilo.
Na Asha Kigundula
MKOA wa Dodoma usiku wa kuamakia leo, umeweka historia mpya pale Mrembo wake Happines Watimanywa kutaoka Kanda ya Kati Dodoma juzi alitangazwa mshindi wa taji la urembo kwa Tanzania maarufu kama Miss Redds 2013 kwenye shindano lilofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City.

Watimanywa alinyakua taji hilo kwa kuwashinda warembo wengine watano walioingia kwenye hatua ya tano bora ambapo mshindi wa pili katika shindano hilo alikuwa Latifa Mohamedi na watatu alikuwa Clara Bayo.


Warembo wengine waliongia katika hatua ya tano bora mbali na washindi hao watatu ni pamoja na Elizabeth Peter na Lucy Tomeka. Kwa ushindi huo ushindi huo Happiness Watimanywa amejinyakulia fedha taslimu shilingi milioni nane na gari yenye thamani ya shilingi milioni  15.


Akitangaza mshindi wa shindano hilo lililoshirikisha jumla ya warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Jaji Mkuu wa Mashindano hayo Dkt Ramesh Shah alisifu warembo walioshiriki kwa mwaka huu na kusema anatarajia mshindi ataiwakilishi nchi vizuri katika mashindano ya dunia mwakani.


“Happiness atakuwa balozi wa Tanzania kwenye mashindano mengi ya kumtafuta mrembo wa Dunia, kama balozi tunaamini ana vigezo vyote vya kuiwakilisha nchi na kuitangaza Tanzania Dunia nzima,”alisema Shah.


Mshindi wa mwaka jana Brigitte Alfred hakuwezi kushiriki shindano hilo kwani yuko Indonesia akishiriki shindano la kumsaka mrembo wa Dunia lakini hata hivyo alitoa ujumbe akiwatakia washiriki mashindano mema.


“Ningependa kuwa na nyinyi kama usiku huu kama ilivyo kawaida lakini sitakuwa nanyi ila nawatakia mashindano mema,”alisema Alfred.


Mrembo huyo wa mwaka wa Tanzania pia alishinda tuzo ya mrembo mwenye mvuto wa picha(Miss Photogenic), Narietha Boniface alishinda tuzo ya mwanamitindo(Top Role Model), Prisca Clement alishinda tuzo ya mrembo kwenye michezo(Top Woman Sports) na Clara Bayo alishinda tuzo ya mrembo mwenye kipaji(Top talent woman) na Severine Lwinga alishinda tuzo ya mrembo mwenye haiba(Miss Personality).


Shindanaao hilo lilipambwa na burudani mbalimbalai kutoka akwa sanii muziki wa kizazi kimya, ambalo limeonekana akuvutia wengi aswa palae alipotangazwa mremboa huyo kutoka mkoa wa Dodoma.


No comments:

Post a Comment