Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Nderakindo Kessy akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari wakati wa
mkutano na uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari-Maelezo leo, jijini Dar es
Salaam.
Katibu wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji akifafanua jambo kuhusu Msimamo
wa wabunge wa Tanzania katika bunge hilo, kuhusu vikao vya Bunge kufanyika kwa
mzunguko, wakati wa mkutano na uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO
leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara
ya Habari Assah Mwambene.
Baadhi wa waandishi wa habari
wakiwasikiliza wabunge wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki
wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari-Maelezo, leo Jijini Dar
es Salaam.
DONDOO
MUHIMU ZA KIKAO NA WAANDISHI WA HABARI 03/09/2013 – MAELEZO
Bunge
la tatu la Afrika Mashariki lilikuta vikao vya Bunge vikifanyika kwa njia ya
mzunguko kwa nchi 4 za Jumuiya ya Afrika Mashariki (Kenya, Uganda, Rwanda,
Burundi) pamoja na Arusha ambayo ni Makao Makuu ya Jumuiya.
Katika
kikao cha Kamati ya Uongozi, Wabunge wa Tanzania walitoa pendekezo kwamba vikao
vya Bunge kwa mwaka huu wa fedha August 2013 –June 2014 vifanyike Arusha, kwa
vile tayari kuna makazi ya kudumu yaani jengo jipya lililojengwa kwa ufadhili
wa Serikali ya Ujerumani na kiwanja kilitolewa na Serikali ya Tanzania.
Hata
hivyo Wabunge wenzetu walipendelea vikao vya Bunge viendelee kwa mzunguko na
Wabunge Watanzania tuliendelea na msimamo wa vikao kufanyika Arusha.
Motion
ililetwa Bungeni na mwenzetu kutoka Kenya kuhusu vikao vya Bunge kufanyika kwa
mzunguko….Spika alimwambia mleta Motion kufuata kanuni ambapo ilitakiwa mjadala
wake uendelee katika kipindi cha masaa 24 baada ya kuwasilisha.
Wabunge
wenzetu hawakukubaliana na uamuzi wa Spika na kuamua kutoka nje na kusababisha
kikao cha Bunge kuahirishwa mpaka siku inayofuata.
Kwa
utaratibu wa kanuni za Bunge, iwapo nchi moja isipokuwa na Wabunge wasiozidi
zaidi ya watu basi kikao cha Bunge kinavunjwa kwa dakika 15 na Bunge kuanza
tena na baada ya hapo ikiwa bado akidi ikiwa haitosh, kikao cha Bunge huvunjwa
mpaka siku inayofuata.
Wabunge
wa Tanzania tuliamua kwa pamoja kuwa na msimamo wa kutoka ndani ya Bunge kwa
kuonyesha kusikitishwa na kitendo cha wenzetu kumdhalilisha Spika wa Bunge
pamoja na kuonyesha msimamo kwamba Wabunge Watanzania vile vile tuna msimamo na
hatukubali kuyumbishwa.
Baada
ya hapo, ndio tuliweza kukaa meza moja na kufikia makubaliano kwamba Arusha
ipate vikao viwili na Tanzania vile vile ipate kikao kimoja. Makubaliano hayo
yalipelekea Motion ya kutaka vikao vifanyike kwa mzunguko kufanyanyiwa
marekebisho ili kuongeza Arusha kupata Vikao viwili na Tanzania kimoja sambamba
na nchi zingine za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kupata vikao kwa njia ya mzunguko.
Vikao
vya Arusha vina umuhimu sana kwani ni Kikao cha Bajeti kitasaidia kupunguza
gharama kubwa kwani wafanyakazi wa Secretariet, Maafisa pamoja na vitabu vya
bajeti na vitendea kazi havitasafirishwa nchi yeyote isipokuwa vitabaki Arusha.
Hali kadhalika kikao cha Ukaguzi vile vile kitapunguza gharama kwa kiasi
kikubwa.
Mhe.
Adam Kimbisa
Mwenyekiti
No comments:
Post a Comment