Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dk. Marina Njelekela (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waliotembelea Kitengo cha Maradhi ya Moyo leo. Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa.
TAARIFA KWA WANANCHI
KUHUSU UBORESHAJI WA HUDUMA MAGONJWA YA MOYO HOSPITALI YA TAIFA MUHIMILI
SEPTEMBA 9, 2013
Awali ya
yote nashukuru kupata fursa hii ya kukutana na vyombo vya habari ili
kuzungumizia baadhi tu ya mafanikio ambayo Hospitali ya Taifa Muhimbili
imeyapata kupitia Kituo cha Upasuaji Moyo na Mafunzo (Cardiac Surgery Treatment
and Training Centre.
Huduma za Upasuaji Moyo:
Kama mnakumbuka tarehe 21 Mei 2008 upasuaji wa moyo ulianza rasmi hapa
Muhimbili, ukifanywa na madaktari wetu baada ya kupata mafunzo nchini
India na Israel. Wagonjwa 105 walifanyiwa upasuaji katika
kipindi cha mwaka mmoja na hadi kufikia leo tayari wagonjwa 453 wameshafanyiwa
upasuaji. Upasuaji wa moyo unaofanyika ni sawa na upasuaji katika vituo vikubwa
vya upasuaji wa moyo duniani kote. Wataalam wetu wamekuwa wakifanya
upasuaji wa kuziba matundu kwenye moyo na
kubadilisha valvu ambazo zimebana na kushindwa kuruhusu damu kupita
kwenye moyo au kulegea na kufanya damu kuvuja kwenda kwenye sehemu isiyohusika katika
moyo na kurudisha moyo katika hali yake ya kawaida ya afya ya mgonjwa.
Pamoja na kufanya upasuaji huduma nyingine ambazo zimefanyika na
zinaendelea kufanyika ni pamoja na kliniki mbalimbali
kama vile za magonjwa ya valve, moyo kupanuka, mishipa ya moyo kuziba, mapigo
ya moyo kushuka, magonjwa ya moyo ya kuzaliwa ya watoto na upasuaji
wa moyo na mishipa ya damu.
Ufungaji wa Vifaa Tiba:
Kituo hiki
kina vifaa vya kisasa na vya hali ya juu na mahsusi kwa ajili ya kumudu
matibabu ya magonjwa makubwa ya moyo. Hospitali inaendelea kutafuta taasisi
zenye uzoefu mkubwa wa matibabu ya moyo ili kuanzisha ushirikiano utakaowezesha
kupata wataalamu wao kuja kushirikiana na wataalamu wetu kutibu magonjwa makubwa
ya moyo hapa hapa nchini kama njia ya kuongeza uwezo kitaaluma. Tunafurahi
kuwaambia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii imetoa fedha kwa ajili ya kununua mtambo mkubwa wa kuchunguza mishipa na shinikizo ndani ya
moyo na maradhi makubwa ya moyo ya kuzaliwa (Catheterization Laboratory). Huu ndiyo mtambo amboa kwa kipindi
kirefu umekuwa ukipelekea Serikali yetu kupeleka wagonjwa wengi wa moyo
kufanyiwa matibabu nchini India. Mtambo huu umefungwa siku za hivi karibuni,
tutaujaribu (testing) mapema mwezi
Oktoba mwaka huu. Mtambo huu umeigharimu Serikali kiasi cha shilingi bilioni 3.6
Jinsi mtambo wa (Catheterization
Laboratory) unavyofanya kazi:
Mtamo huu wa Cath Lab ndio
unaotusaidia kuangalia mishipa ya damu inayoenda kwenye moyo, kuangalia moyo
jinsi unavyofanya kazi na pia kama mtu anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo
mashine au mtambo huu unatusaidia kuangalia vitu mbalimbali kwenye moyo wa mgonjwa
husika ili kujiridhisha kuona kama kuna jinsi yoyote mgonjwa huyu atanufaika na
upasuaji huu. Cath Lab inasaidia pia kuweka kifaa saidizi katika moyo wa mtu
(pacemaker) ambacho ni kama betri kinachosaidia kuufanya moyo ufanye vizuri
siku zote.
Wafanyakazi wa Kituo hiki:
Kituo hiki
kinahitaji wafanyakazi wa kada mbalimbali wapatao 365 lakini kwa sasa kina
watalaam 121. Lakini nafurahi kuwambia kuwa katika mwaka uliopita wa fedha
tulipata kibali kwa ajili ya kuajiri wafanyakazi zaidi ya 100 ili kukidhi
mahitaji halisi ya kituo hiki katika kutoa huduma. Pamoja na hayo tuna changamoto ya
kupata watalaam waliobobea katika
magonjwa ya moyo ambao hawapatikani kwa urahisi katika soko la ajira. Lakini
tunajithaidi kuajiri watalaam ambao tutawapeleka kubobea hususani katika
ubingwa wa nusu kaputi, upasuaji na mishipa ya damu, upasuaji wa moyo kwa
watoto n.k
Gharama za Matibabu:
Kama
mnavyojua, huduma za maradhi ya moyo zina gharama kubwa na zinahitaji wataalamu
wa hali ya juu. Ili huduma hii iwe endelevu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
inapitia upya utaratibu wa kulipia matibabu ikiwa ni na kuzishauri kampuni zote
za Bima ya Afya kulipia wateja wao wanaohitaji huduma mbalimbali za moyo. Kwa
kufanya hivyo Kituo kitaweza kujiingizia kipato kitakachotumika kuboresha
huduma pamoja na kuweka motisha kwa wafanyakazi.
Kituo hiki
kitakuwa faraja kubwa kwa nchi yetu na kitaipunguzia Serikali mzigo
ikizingatiwa kwamba asilimia 70 kati ya wagonjwa wote wanaopata rufaa ya
Serikali kwenda kutibiwa nje ya nchi ni wagonjwa wa moyo. Mathalan serikali kwa makisio inatumia kama dola za kimerakani
10,000 kulipia gharama za matibabu ya mgojwa mmoja nje ya nchi
ukilinganisha na dola za marekani 6,000 mgonjwa akitibiwa
katika kituo chetu cha Moyo Kwa hiyo, kuanzishwa kwa kituo hiki
kutapunguza matumizi ya Serikali kwa kiwango kikubwa sana. Hata hivyo Serikali
inapitia mchakato wa uboreshaji wa utoaji wa huduma pamoja na upatikanaji wa
fedha ili kila Mtanzania aweze kupata huduma bora hapa kwetu.
Uwekezaji Uliofanywa hadi sasa
Ujenzi wa
Kituo hiki umejengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya
Jamhuri ya Watu wa China. Ujenzi pamoja ufungaji wa vifaa hadi hivi sasa
umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 32 ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania imechangia kiais cha shilingi bilioni 16,411,741,367 ambapo
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imechangia shilingi bilioni
15,630,769,600. Uwekezaji huu ni wa dhati na tuna kila sababu ya kuipoingeza
Serikali zote mbili kwa kazi kubwa iliyofanyika hapa.
Mchanganuo wa uwekezaji umebainishwa katika jedwali
lifuatalo;
Na
|
Maelezo
|
Bei kwa Tshs
|
1
|
Msaada wa Ujenzi na kufunga baadhi ya vifaa
kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China
|
15,630,769,600.00
|
2
|
Mchango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa ajili ya ujenzi
|
1,900,000,000.00
|
3
|
Bajeti ya Maendeleo kutoka Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kununua vifaa tiba, mitambo na ufungaji
katika kipindi cha
2010 – 2013
|
11,974,000,000.00
|
4
|
Gharama za Uendeshaji kutoka Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
toka mwaka 2008 – 2012
|
3,400,723,973.00
|
|
Jumla Kuu
|
32,905,493,573.00
|
Utaratibu wa Kutibiwa katika Kituo hiki:
Kituo hiki cha Mafunzo na Upasuaji wa Moyo
kitapokea wagonjwa kupitia mfumo wa rufaa kwa Hospitali zote zilizothibitishwa
kuleta wagonjwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo kundi la kwanza ni
Hospitali zilizoko katika Jiji la Dar es Salaam ambazo ni CCBRT, Lugalo, Amana, Temeke, Mwananyamala, Hospitali binafsi kama Agha
Khan, Hindu Mandal, Kairuki n.k. aidha tutapokea wagonjwa kutoka Hospitali za
Rufaa ngazi ya Kanda kama KCMC, Bugando, Mbeya na Hospitali zote za Mikoa,
Wilaya na Hospitali Teule.
Tumeweka wagonjwa katika makundi matatu yafuatayo;
Wagonjwa wa Msamaha
Kutokana na
Sera ya Msamaha wagonjwa kwa njia hii watachujwa ili kuhakikisha hakuna
matumizi mabaya ya sera hii. Aidha tunaweka utaraitibu mzuri wa kuiomba
Serikali kulipa fedha zote kwa Hospitali kwa wagonjwa wote watakaopewa huduma
kwa njia ya msamaha.
Uchangiaji wa gharama za matibabu
Hapa ndugu
na wanafamilia wa mgonjwa kama ilivyokawaida watatakiwa kuchangia gharama za
matibabu ambapo kiasi kingine kitalipwa na Serikali kuu au Serikali za Mitaa
kulingana na mgonjwa alikotoka.
Wagonjwa wa Kulipia (Private)
Kundi hili
ni kwa wateja ambao wana uwezo wa kulipia fedha taslimu au kupitia bima za
afya mbalimbali ambazo zipo kwa sasa. Baada
ya kusema hayo nawashukuruni sana kwa kunisikiliza.
Asanteni
Dkt. Marina
Njelekela,
MKURUGENZI MTENDAJI,
SEPTEMBA 9, 2013.
No comments:
Post a Comment