TANGAZO


Monday, September 9, 2013

Mbunge wa Korogwe Vijijini, Profesa Maji Marefu afunga mafunzo ya Wajasiriamali Kata ya Mazinde


Mjasiriamali wa Kata ya Mazinde, Amina Shauri akimkabidhi chupa zenye chili sosi Mbunge wa Jimbo hilo, Stephen Ngonyani 'Profesa Maji Marefu', (wa pili kulia), zilizotengenezwa na wajasiriamali wa  kata hiyo waliokuwa kwenye mafunzo ya siku nne, yaliyoendeshwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Happy Business Products ya Jijini Dar es Salaam, ambayo  yaliwashirikisha  wajasiriamali 50 wa kata hiyo. Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji wa  Kata ya Mazinde, Rajabu Mkwizu, Mwewnyekiti wa Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Korogwe, Bakari Mnganzija na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mazinde Rashid Kika. (www.mwaibale.blogspot.com)
Mbunge Ngonyani 'Profesa Maji Marefu', akiwahutubia wananchi wa Kata hiyo.
Wananchi wa Kata ya Mazinde wakiwa katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Korogwe,Bakari  Mngazija akihutubia katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Korogwe, Bakari  Mngazija (kulia), akimkabidhi Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Bernald Mhando sh.200,000, zilizotolewa na Mbunge huyo kwa ajili yakununulia malighafi ya kufundishia mafunzo hayo.
Wananchi wa kata hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo. 
Mbunge Ngonyani 'Profesa Maji Marefu' (kulia), akimkabidhi Rais wa Klabu ya Mpira ya Chicago, Hamad Rashid sh.50,000 kwa ajili ya kununulia mipira ya Klabu hiyo.
Mbunge Ngonyani akimpatia sh.50,000 mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya kiislamu ili ziwasaidie katika mahafali yao yatakayofanyika 
hivi karibuni.
Wasanii wa kikundi cha Shauri cha Kata ya Mazinde wakitoa burudani kwa kucheza ngoma ya Mdumange katika hafla hiyo. Mbunge huyo alitoa zaidi ya sh.100,000 kwa ajili ya wasanii hao.
Vijana wakisakata rhumba la mdumange kwenye hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment