TANGAZO


Saturday, September 21, 2013

Mafunzo ya Haki za Binadamu na Utoaji Haki yatolewa kwa Mahakimu wakazi jijini Dar es Salaam

Naibu Mkurugenzi wa masuala ya Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bi. Sarah Mwaipopo alikuwa miongoni mwa watoa mada katika warsha hiyo. Hapa akiwasilisha mada yake kuhusu wajibu wa Serikali katika utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu nchini. (Picha zote na Germanus Joseph.)
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo.
 Wanawarsha wakiteta jambo wakati wa majadiliano ya vikundi.
Mmoja wa washiriki akiwasilisha taarifa ya majadiliano ya kikundi chake wakati wa mafunzo hayo.
Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria na Haki za Binadamu kutoka Chuo Kikuu cha DSM, Bwana James Jesse, ndiye aliyekuwa Mwezeshaji wa mafunzo hayo. Hapa anaonekena akinukuu michango ya washiriki wa warsha wakati wa majadiliano ya pamoja.
Maafisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi. Caroline Kisunte (kushoto) na Bi. Bitizani Kejo wakifuatilia mada wakati wa warsha hiyo ya mafunzo.
Washiriki wa mafunzo kuhusu haki za binadamu na utoaji haki, mahakimu wakazi kutoka Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB). Mafunzo hayo ya siku tatu yaliandaliwa na THBUB kwa kushirikiana na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Kanda ya Afrika Mashariki, Addis Ababa, Ethiopia. 
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bwana Nabor Assey na Mtaalamu Mshauri  wa masuala ya haki za binadamu kutoka Ofisi ya Kamishna Mkuu wa  Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Meklit Hessebon (katikati) katika picha ya pamoja na mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo yaliyomalizika jana jijini DSM.
Wakiwa wenye nyuso za furaha washiriki wa mafunzo ya haki za binadamu na utoaji haki wakitawanyika kuelekea makwao mara baada ya mafunzo hayo kuhitimishwa.  

No comments:

Post a Comment