Waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Marekani, John Kerry, anakutana na mawaziri wa Jumuia ya Nchi za Kiarabu mjini Paris, akiendelea na ziara yake Bara la Ulaya kutafuta kuungwa mkono kuhusu kuiingilia kati kijeshi nchini Syria.
Hapo awali akiwa pamoja na mwenzake wa Ufaransa, Laurent Fabius, katika mkutano na waandishi wa habari, Bwana Kerry alisema kuwa nchi zaidi zinaunga mkono hatua ya kijeshi dhidi ya Syria kwa kutumia silaha za kemikali mwezi uliopita.
Ufaransa inaiunga mkono Marekani kuhusu Syria, lakini kama wanachama wengine wa Umoja wa Ulaya, inataka kusubiri ripoti ya wachunguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa waliozuru Syria.
No comments:
Post a Comment