Boti moja imezama na kusababisha vifo vya watu 42 katika mto Niger eneo la Kati mwa Nigeria.
Waokozi wangali wanawatafuta watu 100 wanaoaminika kupotea.
Maafisa wanasema kuwa boti hiyo ilizama Ijumaa jioni na huenda ilikuwa imebeba watu wengi kupita kiasi, ikiwa maradufu ya idadi iliyostahili.
Mohammed Shaba, mkuu wa shirika la kushughulikia majanga aliambia shirika la habari la AFP kuwa boti hiyo ilivunjia katikati baada ya kuondoka kutoka kijiji cha Malilli.
Bwana Shaba aliambia shirika hilo kuwa ilikuwa ajali mbaya zaidi kushuhudiwa katika eneo hilo kwa miaka kadhaa.
"Lazima ajali hii iwe funzo kwetu,’’ alisema bwana Shaba.
Alidai kuwa boti hiyo ilikuwa na watu wengi kupita kiasi pamoja na mizigo yao.
Maafisa hata hivyo wanasema maji mengi katika eneo hilo huenda pia yalisababisha ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment