Serikali ya Mali imesema watu ishirini na wanne wameuawa katika mji mkuu wa nchi hiyo Bamako, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha siku ya Jumatano.
Kwa mujibu wa taarifa kutoika kwa wizara ya mambo ya ndani, mvua hiyo ilisababisha mafuriko makubwa na kuwa watu kadhaa walifariki baada ya nyumba zao kuporomoka.
Mwandishi wa BBC mjini humo anasemma kuwa baadhi ya nyumba zilizoporomoka zilijengwa bila idhini katika ardhi iliyotengwa kwa minajili ya kuweka mitaro ya kusafirisha maji machafu.
Anasema magari kadhaa ya usafiri wa umma yalisombwa na mafuriko hayo.
Mafuriko hayo ndio mabaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni nchini humo.
No comments:
Post a Comment