Rais wa Ufaransa amesema uamuzi wa wabunge wa Uingereza wa kuzuia wanajeshi wake kuhusika na mashambulio ya kijeshi nchini Syria, hautabadili azma yake ya kutaka hatua kali kuchukuliwa.
Francois Hollande, amesma wanachunguza kila njia na kuwa huenda wakaishambulia Syria siku chache zijazo.
Matamshi hayo yametolewa muda mfupi baada ya waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel kutangaza kuwa Marekani itaendelea kushirikiana na mataifa mengine, ili kujadili uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Syria.
Serikali ya Marekani imeishutumu Utawala wa Syria kwa kutumia silaha za kemikali, madai ambayo yamepingwa vikali na utawala wa rais Bashar al Assad.
Wakati huo huo, wachunguzi wa Umoja wa mataifa wanaochunguza ikiwa silaha za kemikali zilitumika nchini Syria, wameonekana wakiondoka kutoka hoteli moja moja, ili kutembelea moja katika eneo linalothibitiwa na serikali mjini Damascus.
Wataalamu hao wanatarajiwa kukamilisha kazi hiyo baadaye hii leo na kuwasilisha matokeo yao kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa hiyo kesho.
Katika mahojiano na gazeti moja nchini Ufaransa, rais Hollande alisema kura hiyo katika bunge la Uingereza halijabadilisha uamuzi wake wa kuunga mkono mikakati za kijeshi dhidi ya serikali ya Syria.
Serikali ya Ujerumani pia imesema wanajeshi wake hawawezi kushiriki katika mpango huo wa kuishambuia Syria.
No comments:
Post a Comment