Rais anayemaliza muda wake, Leodegar Tenga. |
DAR ES SALAAM, Tanzania
KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetangaza tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa TFF
na ule wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board), mchakato unaoanzia keshokutwa Agosti 16
kwa wagombea kuchukua fomu kuwania nyadhifa mbalimbali.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hamidu Mbwezeleni, alisema
kuwa Uchaguzi wa Bodi ya TPL, utafanyika Oktoba 18, siku mbili kabla ya
kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa TFF, Oktoba 20, badala ya Septemba 29 ya
awali.
Mbwezeleni alibainisha kuwa, nafasi zitakazogombewa katika
uchaguzi wa TFF ni Rais, Makamu wake na Wajumbe 13 wa Kamati ya Utendaji,
watakaowakilisha kanda tofauti, huku uchaguzi wa Bodi ya TPL ikiwa ni nafasi ya
Mwenyekiti, Makamu na Wajumbe wa bodi hiyo.
Akizungumzia mchakato huo uliosimamishwa awali na Fifa,
Mbwezeleni alisisitiza kuwa, wagombea wanapaswa kuzijua sheria na kanuni
zinazosimamia uchaguzi huo zinazopatikana katika ‘Election Menu’ ya TFF, ili
kujua miongozo na taratibu ili kuondoa malalamiko.
No comments:
Post a Comment