TANGAZO


Sunday, July 7, 2013

Waziri Mkuu Pinda akabidhi tuzo kwa washindi wa Maonesho ya Sabasaba, Barabara ya Kilwa

Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati), akimkabidhi tuzo Mkuu  wa Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania, Dk. Alberic  Kacou ya kutambua mchango wa UN katika jamii ya Kitanzania katika Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati), akimkabidhi  tuzo ya heshima  ya udhamini wa maonesho hayo, Ofisa Masoko wa Nje wa Kampuni ya Tanzania Distilleries  Limited (TDL), Babon Ndumati katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia) akimkabidhi tuzo  Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia  Tanzania (TBL), Emma Orio kwa kutambua mchango wa  kampuni hiyo wa kufadhili sherehe za kufunga Maonesho  ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye  viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati),  akimkabidhi  tuzo ya ushindi wa jumla wa maonesho hayo, Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika  la Mfuko wa Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume katika hafla hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Sabetha Mwambenja, Waziri wa  Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda, Kaimu Mkurugenzi wa Tantrade, Jaqueline Maleko na Mkuu 
wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi tuzo ya  Sekta ya Habari na Mawasiliano, Meneja wa  Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), 
Amini Mbaga katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi tuzo ya  ushindi wa pili wa jumla wa maonesho hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uwekezaji Tanzania (EPZA), Dk. Adelhelm Meru.

No comments:

Post a Comment