TANGAZO


Sunday, July 7, 2013

Rais Dk. Shein: Muungano upo na utaendelea kuwepo

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiwa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili katika Viwanja vya Demokrasia vya Kibandamaiti mjini Unguja katika mkutano wa hadhara wa kuimarisha chama kwa Mikoa ya Unguja leo. (Picha zote na Ramadha Othman, Ikulu)
Katibu wa Idara ya Uenezi wa NEC-CCM Zanzibar, Waride
Bakari Jabu, akihamashisha mkutano wa CCM kwa Mikoa ya Unguja, uliofanyika leo, Uwanja wa Demokrasia wa Kibandamaiti, Mjini Zanzibar katika mkutano huo, wanachama wa chama hicho, waliofurika kwa maelfu na pia kuhudhuriwa na Rais mstaafu wa Zanzibar, Komando, Dk. Salmin Amour Juma.
Makamu Mwenyekiti na Rais mstaafu wa Zanzibar,
Komandoo, Dk. SAlimin Amour Juma, (wa pili kushoto), akifuatana na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mjini, Borafya Silima Juma (kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamo wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda maiti katika mkutano wa hadhara wa kuimarisha chama kwa Mikoa ya Unguja leo.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamo Mwenyekiti na Rais mstaafu wa Zanzibar, Komandoo Dk. Salimin Amour Juma, alipoasili katika mkutano wa CCM, uliofanyika leo, katika Viwanja vya Demokrasia wa Kibandamaiti, mjini Unguja katika mkutano wa hadhara wa kuimarisha chama, Mikoa ya Unguja  leo.
Wanachama wa CCM wa maskani ya Kisonge, wakishangilia
katika mkutano wa hadhara, uliofanyika leo na kuhutubiwa na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, Uwanja wa Kibandamaiti Mjini Zanzibar.
Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais mstaafu wa Zanzibar, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Komandoo Dk. Salmin Amour Juma, alipokuwa akiwasalimia na kuwahutubia wanachama na wananchi katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Demokrasia, Kibandamaiti, mjini Zanzibar. 
Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais mstaafu wa Zanzibar, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Komandoo Dk. Salmin Amour Juma, akiwahutubia wanachama na wananchi katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Demokrasia, Kibandamaiti, mjini Zanzibar leo. 
Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais mstaafu wa Zanzibar, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Komandoo Dk. Salmin Amour Juma, akihutubia mkutano huo wa hadhara katika Uwanja wa Demokrasia, Kibandamaiti, mjini Zanzibar leo. 
Wanachama wa CCM wa maskani mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo, wakimsikiliza Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, Uwanja wa Kibandamaiti, Mjini Zanzibar leo.
Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM wa Mikoa ya Unguja, katika mkutano wa kuimarisha chama chake, Viwanja vya Demokrasia, Kibandamaiti mjini Zanzibar leo. Katika mkutano huo, Rais Shein alizungumzia uwepo wa Serikali mbili, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano wa Tanzania. 

Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM wa Mikoa ya Unguja, katika mkutano wa kuimarisha chama chake, Viwanja vya Demokrasia, Kibandamaiti mjini Zanzibar leo. Katika mkutano huo, Rais Shein alizungumzia uwepo wa Serikali mbili, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano wa Tanzania. 

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza kuwa Muungano upo na utaendelea kuwepo na kusisitiza kuwa msimamo wa CCM ni Serikali mbili.
 Dk. Shein aliyasema hayo leo huko katika viwanja vya Demokrasia, Kimandamaiti mjini Zanzibar wakati akiwahutumia maelfu ya Wana CCM na wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema kuwa hivi sasa kumekuwepo maelezo mengi ya upotoshaji juu ya Muungano ambayo aliyaeleza kuwa hayana msingi na kusisitiza kuwa mabadiliko ya Katiba Mpya ni kuimrisha Muugano na wala si kuuvunja.

Dk. Shein aliwaeleza wanaCCM na wananchi juu ya mchakato mzima wa Katiba unavyoendelea hivi sasa na kusisitiza kuwa hakuna wa kuwasemea Wazanzibari na badala yake watasema wenyewe wakati ukifika kwenye kura ya maoni.

Alisema kuwa amekaa kimywa kwa mwaka mmoja sasa, na kilichomchukiza kile cha kumgombanisha na wanaCCM wenzake na wananchi anaowaongoza,

Dk Shein alitoa maelezo juu ya Kamati ya Maridhiano ambayo imekuwa ikitoa vizingizio kuwa yeye ameibariki.

Alisema kuwa msimamo wa CCM ni wa Serikali mbili na si vyenginevyo kwani huoi msimamo wake na wala hatomzuia mtu na msimamo wake na kukemea kutoingizwa katika mambo menie

“Wamelipika wenyewe walinywe wenyewe.. wasitake kupanda mabega ya Serikali kupitia kwangu na nawahakikishia wanaCCM kuwa  ataendelea mimi nitaendelea kuwatetea wananchi wote’” ALISEMA Dk. Shein.




Dk. Shein alisema kuwa “CCM iko imara na wapo waliodhani kuwa CCM ilikuwa likizo na si kweli tulikuwa tukijiandaa katika kuwachagua viongozi wetu kuanzia  Mashina hadi Taifa”.

Wakifanya moja tufanye mitano wakifanya asubuhi tufanye jioni wakifanya Jumaamosi sisi tufanye Jumaapili… tunataka kasi hii iendelee hadi 2015”,alisisitiza Dk. Shein.

Aliwataka wanaCCM kujiandaa na kuongeza WanaCCM na kueleza  kuwa zaidi ya elfu tano na kueleza kuwa ni kazi ya CCM kuwashajiisha watu kujiunga na CCM.

Alisisitiza kuwa amani haina mbadala na Serikali yake anayoiongoza haitna mzaha katika kuimarisha amani.

Alieelza kuwa hatomuogopa na kumchelea mtu yoyote atakaevunja amani ya nchi na kusisitiza kuwa hakuna utani katika kuimarisha amani.

Alieeleza kuwa maamuzi ya Zanzibar yanafanywa Zanzibar na sivyo inavyoelezwa kuwa yanaamuliwa Dodoma na kusema kuwa Serikali inaongozwa kwa Katiba na Sheria za nchi ziliopo. “Na asitokee mtu akasema mie simo mie simo sote tumo kwani sote tunakauli moja ya kuongoza Zanzibar.

Alieelza kuwa anawaamini wale wote, na kueleza kuwa atakaekwenda kinyume na maamuzi na taratibu za serikali atachukua hatua.

Dk. Shein alieelza mafanikio yaliopatikana katika serikali anayoipngoza huku akiahidi kuongeza mishahara mwaka huu kwa wafanyakazi wote wa Serikali.

Alisema kuwa hayo yote yanawezekana iwapo wananchi wataanzisha miradi yao ya maendeleo na hatimae serikali kuwaunga mkono.

Aidha, Dk. Shein alieelza kuwa CCM itaendelea kuwa imara zaidi kwani kasi yake ni kubwa sana huku akieleza jinsi alivyojionea katika ziara zake za Chama alizofanya katika mikoa yote ya Unguja na Pemba .

Akitoa salamu zake, Rais mstaafu wa Zanzibar Dk. Salmin Amour Juma maarufu Kamandoo, alisema kuwa umoja wa WanaCCM utadumu na chama kitadumu na Afrika itadumu.

Alieeleza kuwa vijana ndio ngao na ngome ya chama hicho na kuwapongeza akina mama ambao ndio waliokuwa wakibeba watoto migongoni na kusimamia ASP na TANU na kueleza kuwa wazee wataendelea kujikongoja na kusema kuwa yeye hajambo na yuko imara..

Nae Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alitoa Shukurani kwa Dk. Salmini kwa kutoa ahadi ya kuja katika mkutano huo na kuweza kuhudhuria na kueleza kuwa CCM imejidhatiti na kutoa misimamo yake katika masuala mbali mbali ya maendeleo na Muungano.

Katika  risala ya wanaCCM wa Mikoa sita ya Kichama, walieleza kuwa Madhumini ni kukipongeza chama cha CCM na kumpongeza Rais Kikwete na Rais Dk. Shein na kueleza kuwa chama hicho kitaendelea kuwa darasa kwa vyama vyengine.

Risala hiyo ilieleza kuwa Tanzania inaendelea kuwa ni nchi ya amani na utulivu na kuwa nchi yenye maendeleo endelevu na kuwa kioo kwa nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara.

Ilieleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitumia kisingizio cha Katiba mpya kwa kufanya vitendo vilivyo nje ya maadili na kupandikiza chuki na kuwagawa watu kwa maeneo wanayotoka.

Risala hiyo pia, ilieleza mafanikio ya Muungano huku ikieleza kuwa kero zote ndani ya Serikali mbili zinatatulika ikifananishwa na mifumo myengine ya Serikali.

“Kuwepo kwa changamoto ni vitu visivyoepukika, hakuna Nkataba, hakuna moja wala tatu ni mbili tu”, ilieleza risala hiyo.

Kamati Maridhiano ya CUF na CCM hawaitambui na hawajui meundwa vipi na kueleza kuwa ni kamati ambayo haiitakii mema CCM.

Katika mkutano huo viongozi mbali mbali wa CCM walihudhuria akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais mstaafu wa Zanzibar Dk. Salmin Amour Juma.

No comments:

Post a Comment