Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifafanua jambo wakati wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba. (Picha zote na Frank Shija)
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia kulia ni Mwakilishi wa Kampuni ya China Power Investment ambaye jina lake alikupatikana.
Pichani aliyekaa kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba kiweka saini mkataba wa makubalianokuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia, waliosimama kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa China hapa nchini Balozi Lu Youqing na Rais wa Kampuni ya China Power Investment, Lu Qizhou.
Baadhi ya wajumbe kutoka Kampuni ya China Power Investment wakifuatilia zoezi la uwekaji saini mkataba wa makubaliano kuhusu uzalishaji umeme kwa mradi wa Kinyerezi III wenye uwezo wa kuzalisha umeme mega wati 600 kwa kutumia gesi asilia.
Na Frank Shija – Maelezo
SERIKALI imesema kuwa kugundulika kwa gesi asilia yenye mita za ujazo takribani milioni 41.7 katika maeneo mbalimbali nchini kunafanya Tanzania kuingia katika taswira mpya katika kujenga uchumi wake.
Kauli hiyo imetolewa leo, jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo wakati wa hafla kutiliana saini mkataba wa makubaliano baina ya Tanesco na Kampuni ya China Power Investement kwa ajili ya mradi wa kuzalisha umeme kwa pamoja.
Profesa Muhongo amesema kuwa kuanzishwa kwa mradi huo wa uzalishaji wa umeme kwa ushirikiana na Kampuni kutaongeza thamani ya rasilimali ikiwemo gesi kwa kuwa uzalishaji wa umeme katika mradi huo utatumia gesi asilia.
Waziri huyo aliongeza kuwa umeme utakaozalishwa utatumika kwa matumizi ya ndani na ziada itauzwa nje ya nchi ili kuletea Taifa mapato na kukuza uchumi wake ambapo mapato hayo yatasaidia Serikali kujitegemea kwa kiasi kikubwa katika bajeti yake.
“Kupitia miradi ya uzalishaji umeme kama hii taifa letu sasa linaonyesha matumaini nahii ni dalili kwamba rasilimali tulizonazo zimeanza kutunufaisha sote, pindi mradi huu ukikamilika tutakuwa na uhakika wa umeme na maana yake uchumi wetu hautakuwa tegemezi tena”.Alisema Profes Muhongo.
Aidha Muhongo alisema kuwa hadi kufikia 2017 jumla megawati 1800 itakuwa imezalishwa kama umeme wa ziada, na hivyo kuweza kuuza nje ya nchi na kujipatia kipato.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kuwa kupitia utaratibu wa ushirikishaji wa taasisi za umma na binafsi katika kutoa huduma za kijamii ndiyo ulioleta mafanikio ya kupata mradi huo ambao Tanesco na Kampuni ya China Power Investnment wameingia makubaliano ya kuzalisha umeme kwa pamoja.
Mhandisi Mramba aliongeza kuwa mradi wa uzalishaji umeme wa Kinyerezi namba III utazalisha umeme jumla ya mega wati 600 pindi utakapo kamilika.
Serikali kupitia Shirika lake la Usambazaji na Uzalishaji umeme (TANESCO) imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili kufikia malengo yake katika kuhakikishia jamii inapata umeme wa uhakika na kwa gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment