Kikosi cha Yanga kilichopambana na Simba katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom,Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo.
Mashabiki wa Simba , mmoja akiwa amevalia kinyago cha mnyama huyo, wakishangilia timu yao katika mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga wakiwa na mfano wa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom, wakionesha ishara ya kumchinja mnyama katika mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga, wakionekana kana kwamba ni mtu na mkewe, wakionesha vimbwanga uwanjani kabla ya mchezo kuanza.
Mashabiki wa Yanga wakiwa na kinyago chao wakifurahia timu yao, uwanjani hapo kabla ya mchezo kati ya timu yao hiyo na Simba kuanza.
Shabiki wa Simba akionesha kibao chenye maandishi yanayosomeka Simba 2 Yanga 0.
habiki wa Yanga akiwa ameng'ata nyama akionesha kwamba timu yake hiyo leo itaibuka na ushindi.
Vijana wakiingia uwanjani kwa kuchupa ukuta wa uwanja kutokana na wingi wa watu waliokuwa wakiingia kwenda kuona mchezo huo.
Wachezaji wa Simba na Yanga wakipeana mikono, wakati wapokuwa wakisalimiana kabla ya mchezo baina yao kuanza leo jioni.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo, dhidi ya Simba lililofungwa na Didier Kavumbagu katika dakika ya tano kipindi cha kwanza.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia wakiwa na Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, walilokabidhiwa baada ya kuwafunga watani wao wa jadi Simba mabao 2-0, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Wachezaji wa Yanga wakiwa wamelinyanyua juu Kombe la Ubinwa wa Ligi Kuu ya Vodacom, mara baada ya kukabidhiwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
|
No comments:
Post a Comment