TANGAZO


Saturday, May 4, 2013

Rais Dk. Shein awaapisha Mwenyekiti, Wajumbe wa Tume Uchaguzi Zanzibar, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha.
Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Balozi Ramadhan Omar Mapuri.
 Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Salmin Senga Salmin.
Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar,  Nassor Khamis Mohamed.
Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jaji Abdulhakim Ameir Issa.
 Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Ayoub Bakari Hamad.
 Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Haji Ramadhan Haji.
 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dk. Idris Muslim Hija.

Makamo wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,  Pandu Ameir Kificho wakiwa katika hafla ya kuwaapisha Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Unguja Ikulu, Mjini Zanzibar leo. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini na Kadhi Mkuu wa Zanzibar,  Sheikh Khamis Haji, wakiwa katika sherehe ya kuwaapisha Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Mwenyekiti wake pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na viongozi waliohudhuria katika sherehe ya kuwaapisha Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Mwenyekiti wa tume hiyo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akimwapisha Jecha Salim Jecha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu, Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Balozi Omar Ramadhan Mapuri, kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Nassor Khamis Mohamed, kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Salmin Senga Salmin, kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Ayoub Bakari Hamad, kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Jaji Abdulhakim Ameir Issa, kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Haji Ramadhan Haji, kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Dk. Idris Muslim Hija, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wakuu,pia wakiwemo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar(wa pili kushoto)na wajumbe wa tume hiyo, akiwemo  Mkuu wa Mkoa kusini (waliosimama kulia)baada ya hafla ya kiapo Ikulu Mjini Zanzibar. 



Said Ameir, Ikulu Zanzibar 
Mei 4, 2013                                                     
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amemuapisha Jecha Salim Jecha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar na wajumbe wa Tume hiyo.

Wajumbe wa Tume hiyo, walioapishwa ni Balozi Omar Ramadhani Mapuri, Salmin Senga Salmin, Nassor Khamis Mohammed, Ayoub Bakari Hamad, Jaji Abdulhakim Ameir Issa na Haji Ramadhani Haji.

Katika hafla hiyo iliyofanyika leo, Ikulu Zanzibar Rais pia alimuapisha Dk. Idris Muslim Hija kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi Khamis, Mufti wa Zanzibar,  Sheikh Saleh Omar Kabi na Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khamis Haji Khamis.


No comments:

Post a Comment