TANGAZO


Friday, May 3, 2013

Majambazi 5 wauawa katika mapambano na Jeshi la Polisi Mbeya

Miili ya majambazi 5 waliouawa katika mapambano na Jeshi la Polisimkoani Mbeya leo, wakiwa wamehifadhiwa Hositali ya Rufaa ya Mbeya. (Picha zote na Venence Matinya)


Polisi wakiwaonesha waandishi wa habari majambazi yaliyouawa na jeshi hilo.


Miili ya majambazi 5, waliouawa katika mapambano na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya leo, wakiwa katika chumba maalum cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.


Mkuu wa Kikosi cha Polisi akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu tukio la majambazi hao.



Mkuu wa Kikosi cha Polisi akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu tukio la majambazi hao. 



Na Venance Matinya, Moses Ng’wat, Mbeya.
MTANDAO wa Ujambazi nchini hususani mkoani Mbeya, umezidi kusambaratishwa  baada ya watu watano wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kuuawa katika majibizano na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani amewaambia wandishi wa habari ofisini kwake, kuwa tukio hilo lilitokea leo, majira ya saa sita mchana katika kijiji cha Garijembe, Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.
Alisema kuwa Jeshi la Polisi lilipata taarifa za kiintelijensia na kuweka mitego mbalimbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao, wakiwa kwenye gari lenye  namba za usajili T  911 BUG, aina ya Toyota Spacio baada ya kusimamishwa katika eneo hilo, wakitokea Kyela kuelekea Jijini Mbeya.
Alisema kuwa baada ya kusimamishwa ghafla, walianza kurusha risasi ovyo  ambapo askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano, ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.
Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na silaha mbili, ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628, ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III, yenye namba 94695J, ikiwa na risasi mbili pamoja na koa za shaba.
Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za kiintelijensia zilieleza kuwa majambazi hayo, yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini, wilayani Rungwe pamoja na eneo la Uyole Jijini Mbeya.
Aidha, alisema majina yao wala makazi yao, hayakuweza kujulikana mara moja ambapo miili yao, imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao, ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.
Pia alitoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu, kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.

No comments:

Post a Comment