TANGAZO


Wednesday, April 10, 2013

Sherehe za Kuapishwa Uhuru Kenyatta, Uwanja wa Kasarani nchini Kenya, Rais Kikwete na wenzake wahudhuria


Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania na mkewe, mama Salma, wakiwasili kwenye Uwanja wa Kasarani kuhudhuria kuapishwa Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta na kukabidhiana madaraka rasmi na Rais anayemaliza muda wake, Mwai Kibaki jana. Marais wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Museven wa Uganda, Kabila wa DRC, Kagame wa Rwanda na Rais mstaafu wa Zambia, Keneth Kaunda. (Picha na Ikulu)

Kikosi cha Wanamaji wa Jeshi la Kenya wakiwa katika gwaride la sherehe hizo jana. (Picha na BBC Swahili)


Kikosi cha Jeshi la Polisi la Kenya kikiwa katika gwaride la sherehe hizo jana.

Kikosi cha Pikipiki cha Askari wa Usalama barabarini nchini Kenya wakipita kwenye Uwanja wa Kasarani kumuongoza Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta (nyuma yao), wakati akiwasili kwenye Uwanja huo jana tayari kwa kuapishwa na kukabidhiwa madaraka ya Urais rasmi.


Kikosi cha Jeshi la Ulinzi la Kenya kikiwa katika gwaride la sherehe hizo jana.


Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta, akilakiapo rasmi cha kuwa Rais wa Nne wa nchi hiyo jana.


Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwa ameshikilia hati za kiapo chake cha kuwa Rais wa nne wa nchi hiyo, mara baada ya kula kiapo jana.


Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta akizionesha hati za kiapo chake cha kuwa Rais wa nne wa nchi hiyo, mara baada ya kula kiapo uwanjani hapo jana.



Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta, akiuangalia upanga aliokabidhiwa na Rais anayemaliza muda wake, Mwai Kibaki (kushoto), ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa madaraka rasmi baada ya kuapishwa uwanjani hapo jana.


Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta, akiuonesha upanga kwa wananchi na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo uwanjani hapo mara baada ya kukabidhiwa na Rais anayemaliza muda wake, Mwai Kibaki (wa pili kushoto), ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa madaraka rasmi.

Rais Jakaya Kikwete na mkewe, mama Salma, Rais wa Rwanda, Paul Kagame na baadhi ya viongozi wengine wa sasa na wastaafu wa Afrika, wakiwa katika sherehe hizo, uwanjani hapo jana. Kulia ni Rais mstaafu wa Awamu ya Pili nchini Kenya, Daniel Arap Moi. (Picha na Ikulu)
Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwapungia wananchi wa Kenya waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwake, Uwanja wa Kasarani jana.
Rais Jakaya Kikwete na mkewe, mama Salma, wakibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waliohudhuria hafla hiyo, uwanjani hapo.

Rais mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta (wa tatu kushoto), wakizungumza jambo na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto pamoja na familia zao, Ikulu nchini humo mara baada ya kula kiapo na kukabidhiwa rasmi madaraka ya Urais na Rais alliyemaliza muda wake, Mwai Kibaki, Uwanja wa Kasarani jijini Nairobi  jana. 

No comments:

Post a Comment