Waumini wa Dini ya Kiislam wakisoma hitima kumuombea marehemu Hajjy Mohammed katika Msikiti wa Nambar Muembetanga, asubuhi ya leo kabla ya kuswaliwa maiti, ikiongozwa na Sheikh Nurdini. (Picha zote na Othman Maulid wa Zanzinews)
Waumini wa dini ya Kiislam wakiuswalia mwili wa marehemu Hajjy Mohammed Omar katika Msikiti Nambari, Muembetanga.
Waumini wa Kiislam wakiuombea dua mwili wa marehemu Hajjy Mohammed Omar, mara baada ya kuuswalia katika Msikiti wa Nambari, Muembetanga.
Waombolezaji na waumini wa dini ya Kiislam wakiuombea dua mwili huo.
Jeneza lenye mwili wa Hajjy Mohamed, likitolewa msikitini kwa ajili ya kupelekwa makaburini kwa mazishi leo asubuhi, Kijiji cha Shakani kisiwani Zanzibar.
Waombolezaji wakilibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Hajjy Mohammed, wakati likiwa katika maeneo ya michezani kwa ajili ya kwenda makaburi katika kijiji cha Shakani kwa ajili yamaziko leo asubuhi.
Waombolezaji wakiuzika mwili wa marehemu Hajjy Mohamed kwenye makaburi ya Kijiji cha Shakani, kisiwani Unguja leo.
Waombolezaji wakimalizia kuuzika mwili wa marehemu Hajjy Mohamed kwenye makaburi ya Kijiji cha Shakani, kisiwani Unguja leo.
Waombolezaji wakiwa kwenye mazishi ya Mkurugenzi wa 'The East African Melody', marehemu Hajjy Mohamed kwenye makaburi ya Kijiji cha Shakani, kisiwani Unguja leo.
Msanii na Mkurugenzi wa kundi la Jahazi, Mzee Yussuf, akiweka mti kwenye kaburi la marehemu Hajjy Mohamed, wakati wa mazishi hayo.
Baadhi ya wasanii alikuwa pamoja nao marehemu Hajjy Mohamed kwenye kundi la Melody, wakimuombea dua marehemu huyo.
Waombolezaji wakiomba dua mara baada ya kuuzika mwili wa marehemu Hajjy Mohamed kwenye makaburi hayo. Kushoto ni mtoto wa kwanza wa marehemu Hajjy Mohamed.
Waombolezaji wakimnyamazisha na kumliwaza mtoto wa kwanza wa marehemu Hajjy Mohamed mara baada ya kumalizika mazishi baba yake leo.

No comments:
Post a Comment