Mkurugenzi wa Kikosi cha Maji kutoka Nigeria, Meja Jenerali Ati John (kushoto), akimwelezea jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sethi Kamuhanda kuhusu picha ya kinyago kinachoonyesha mtawala wa makabila mbalimbali ya nchi hiyo, alipomtembelea ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.Jumla ya wanajeshi 22 kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha Nigeria, wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku tano.
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sethi Kamuhanda (kulia), akimkabidhi picha ya wamasai, Mkurugenzi wa Kikosi cha Maji kutoka Nigeria, Meja Jenerali Ati John, wakati wanajeshi 22 kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha jeshi, walipomtembelea ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sethi Kamuhanda (kulia), akimkabidhi picha ya kinyago cha ujamaa, Mkurugenzi wa Kikosi cha Maji kutoka Nigeria, Meja Jenerali Ati John, wakati wanajeshi 22 wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha Nigeria, walipomtembelea ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam. Wanajeshi hao, wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku tano nchini.
Kanali Anderson Msuya (kushoto), kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), akiongea jambo na Mkurugenzi wa Kikosi cha Maji kutoka Nigeria, Meja Jenerali Ati John, wakati wanajeshi 22 kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu, walipoitembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Mchezo leo, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanajeshi 22 kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha Nigeria, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sethi Kamuhanda (hayupo pichani) wakati walipomtembea ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza nchini, Joyce Fisoo, akielezea kuhusu kazi za bodi hiyo kwa wanajeshi 22 kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha jeshi la Nigeria, walipoitembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Joyce Hagu ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utamaduni.
Wanajeshi 22 kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha jeshi la Nigeria, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, wakati walipoitembelea wizara hiyo leo, jijini Dar es Salaam. Wanajeshi hao kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu jeshini, wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku tano.
Na Magreth Kinabo
"ELIMU ya uzalendo imesaidia
kuwafanya vijana wa Kitanzania kuipenda nchi yao, hali
iliyochangia nchi yetu kuwa na amani na utulivu".
Kauli hiyo, ilitolewa leo na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na
Michezo,Seth Kamuhanda wakati akizungumza na ujumbe wa watu
22,baadhi yao ni viongozi wa utawala na 13 ni wanafunzi wa Chuo cha Ukamanda
na Unadhimu wa mafunzo ya kijeshi kutoka Nigeria.
Ujumbe huo umetembelea wizara
hiyo kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali ya Utamaduni wa
Kitanzania, umeongozwa na kiongozi wa msafara, Meja Generali,
Ati John,ambaye ni Mkurugenzi wa Jeshi la Wanamaji.
“Mojawapo ya program
tunazowafundisha vijana ili kuondoa migogoro katika
nchi yetu ni elimu ya uzalendo ,yaani tunawafundisha jinsi ya kuipenda
nchi yao. Elimu hii imesaidia kupunguza migogoro,alisema.” Katibu
Mkuu huyo alipokuwa akijibu swali la mmoja ya wanafunzi hao
lililouliza kuwa kuna program zipi zinazochangia kupunguza
migogoro hususan kwa vijana.
Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa
kuna mkakati wa kuwawezesha vijana kiuchumi ili waweze kubuni miradi
mbalimbali kwa kuwa na mfuko wa vijana.
Alisema katika mpango huo vijana
wanakuwa katika vikundi na kufanya shughuli mbalimbali
kuwawezesha kiuchumi.
Aidha Katibu Mkuu huyo
akizungumza kuhusu masuala ya kiutamaduni ,alisema wizara yake ndi
yenye jukumu lakuendeleza Utamaduni wa Mtanzania, hivyo katikawizara hiyo
yenye sekta nne, ambazo ni Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Kamuhanda alisema
sektaya utamuduni ndio inayofanyakazi ya kudumisha Utamaduni huo.
Aliongeza kuwa lugha ya
Kiswahili ndio imekuwa lugha kuu ya mawasiliano nchini na ndiyo
iliyoleta umoja ,amani na mshikamano.
Wakizungumzia kuhusu ziara
hiyo kiongozi huyo na mmoja wa wanafunzi, Ikema Francis walisema
wameshukuru kwa taarifa walizopata kuhusu wa masuala hayo ya kiutamaduni na
kuhafamu kuwa lugha ya Kiswahili ndiyo imeleta umoja.
|
No comments:
Post a Comment