TANGAZO


Saturday, February 9, 2013

Serikali ya Tunisia yaitisha maandamano


Chama tawala cha Kiislamu cha Tunisia, Ennahdha, kmeitisha maandamano leo katika mji mkuu, Tunis, baada ya umati mkubwa kuhudhuria mazishi ya kiongozi wa upinzani, Chokri Belaid.
Maandamano yaliyopita ya mjini Tunis
Katika ukurasa wake wa Facebook, chama cha Ennahdha kimewaomba watu wakusanyike saa nane za mchana kulitetea bunge halali ya nchi na kupinga ghasia za kisiasa.
Huu ndio wito wa kwanza wa maandamano kwa wafuasi wa chama tawala tangu Bwana Belaid kuuwawa siku ya Jumaatano.
Waandamanaji katika mazishi yake Ijumaa, waliilaumu Ennahdha kwa mmauaji yake.
Polisi walifyatua moshi wa kutoza machozi wakati baadhi ya waandamanaji walipochoma moto magari wakitaka mapinduzi mepya.

No comments:

Post a Comment