TANGAZO


Sunday, February 10, 2013

Mkutano wa CHADEMA kupinga maamuzi ya Spika wa Bunge, Temeke Mwisho, jijini Dar es Salaam

Viongozi wa juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiwa kwenye mkutano wao wa kupinga baadhi ya maamuzi yaliyotolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anna Makinda, bungeni hivi karibuni, ikiwemo kuivunja Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na maamuzi mengine. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Mbunge wa Kawe, jijini Dar es Salaam, Halima Mdee, akihutubia katika mkutano huo, uliofanyika leo, Temeke Mwisho. 

 Wanachama pamoja na wananchi wakiwa kwenye mkutano huo, wakiwasikiliza viongozi wakuu wa chama hicho leo jioni.

Moja ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na wanachama na mashabiki wa Chama hicho, kwenye mkutano huo, likiwaonya Spika Makinda na Msaidizi wake, Job Ndugai, likioneshwa kwa waandishi wa habari.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, akihutubia mkutano huo.

Mwenyekiti wa CHADEMA), Freeman Mbowe (kulia), Katibu Mkuu, Wilbroad Slaa (katikati) na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika wakiteta jambo wakati wa mkutano huo.

Mbunge wa Arusha Godbless Lema, akitoa namba za simu za Spika Makinda kwa wanachama na mashabiki wa Chama hicho, kwa ajili ya kumtumia meseji za kumtaka ajirekebishe ama kuachia ngazi ya madaraka yake hayo.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, akitoa namba za simu za Naibu Spika, Job Ndugai kwa wanachama na mashabiki wa Chama hicho kwenye mkutano huo kwa ajili ya kumtumia meseji za kumtaka ajirekebishe ama kuachia ngazi ya madaraka yake hayo.

 Katibu Mkuu wa Chadema, Wilbroad Slaa, akihutubia mkutano huo.

Wanachama na mashabiki wa chama hicho wakifuatilia hotuba za viongozi wao wakuu kwenye mkutano huo Temeke Mwisho, jijini Dar es Salaam leo.

 Mwenyekiti wa CHADEMA), Freeman Mbowe, akihutubia mkutano huo, ambapo pamoja na mambo mengine aliwaelezea wanachama wa chama hicho, kwamba wakigombane na wanacha wa vyama vingine bali wawaelimishe ili waungane nao katika kukiimarisha chama hicho.

Baadhi ya Wabunge na wanachama waandamizi wa chama hicho wakiwa kwenye mkutano huo.

Baadhi ya Wabunge na wanachama waandamizi wa chama hicho, wakifutilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na viongozi wao wakuu wa chama kwenye mkutano huo.

No comments:

Post a Comment