TANGAZO


Monday, February 11, 2013

Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, mjini Dodoma leo


Mwenyekiti wa Chama Cha Mpinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, akizungumza wakati alipokuwa akikiongoza kikao cha NEC, kwa kuendelea na semina jana na leo, ukumbi wa White House, Mako Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdurrahaman Kinana. 
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akizungumza wakati alipokuwa akikiongoza kikao cha NEC, kwa kuendelea na semina jana na leo, ukumbi wa White House, mjini Dodoma. 
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiteta jambo na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Zakia Meghji, kabla ya kuanza kikao hicho leo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akimsikiliza Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Zakia Meghji. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, kabla ya kikao kuanza leo.
Mjumbe wa NEC, Mama Salma Kikwete, akisalimiana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (wa pili kulia), kabla ya kikao kuanza ukumbini. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Hali ndani ya ukumbi ilikuwa kama hivi kabla ya kikao kuanza. Kushoto Kabisa ni Nape na Zakia Meghji na juu kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na wajumbe wa NEC, kulia chini ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhamed Seif Khatib na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakiteta jambo.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai kabla ya kikao kuanza, mjini Dodoma leo. 
Wajumbe wa NEC, Profesa Anna Tibaijuka na Mzee Mtandika, wakibadilishana mawazo ukumbini humo leo.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akizungumza jambo na Mjumbe wa NEC, Samwel Sitta na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia), kabla ya kikao leo.
Nape Nnauye (kulia), akichangia kwenye mazungumzo hayo kati yake na Dk. Asha-Rose na Samwel Sitta.
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, ambaye sasa ni Mjumbe wa NEC, Wilson Mukama, akibadilishana mawazo na mjumbe mwenzake wa NEC, Profesa Juma Kapuya, ukumbini hapo.
Hii ndiyo Sekretarieti inayofuatilia na kuweka kumbukumbu ya mijadala mbalimbali, inayozungumzwa kwenye mkutano huo.
Mjumbe wa NEC, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto), akiteta jambo na Mzee Mtandika kabla ya kuanza kikao hicho leo.
Katibu Mkuu wa UWT, Sophia Simba akijadiliana jambo na wajumbe wenzake wa NEC, Amina Salim Ali (kushoto) na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Ana Makilagi, ukumbini hapo. 
 Dk. Asha-Rose Migiro, akimweleza jambo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
Dk. Asha-Rose Migiro, akimfahamisha jambo Nape Nnauye, wakati wa mazungumzo yao hayo, ukumbini humo kabla ya kikao.
Katibu wa Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib (kushoto), akifurahia jambo, wakati alipokuwa akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, kabla ya kikao kuanza.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa, Alhaj Abdallah Bulembo (kushoto), akiwasalimia wajumbe wenzake wa NEC, ukumbini humo, kabla ya kikao kuanza leo.
 Baadhi ya wajumbe wa NEC, wakisubiri kwa hamu, kuanza kwa kikao hicho leo.
Makamu wa Rais, Dk. Muhammed Gharib Bilal (kulia) na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili), wakiwa katika safu ya mbele na baadhi ya wajumbe wengine kwenye kikao hicho leo.
Baadhi ya wajumbe wakipitia nyaraka muhimu kabla ya kuanza kwa kikao hicho.
Aliyekuwa Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma a.k.a Mama Mshua (kulia), akimsalimia Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabiba nje ya ukumbi huo. Katikati ni Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba anaonekana akizungumza jambo na Mjumbe wa NEC, aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu walipokutana nje ya ukumbi kabla ya  kuanza kwa kikao hicho leo.
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Wilson Mukama (kushoto), akimweleza jambo, Mjumbe wa NEC, Steven Wasira, nje ya ukumbi huo leo.
Wajumbe wa NEC, wakiangua kicheko cha kutaniana kaba la kuingia ukumbini kwa kikao, mjini Dodoma leo. Kutoka kushoto ni Dk. Rafael Chegeni, Januari Makamba, Halimenshi Mayonga na Samwel Sitta.
Wajumbe wakiwa tayari kuingia ukumbini kwa ajili ya kuanza kikao chao leo. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

No comments:

Post a Comment