TANGAZO


Wednesday, January 9, 2013

Viongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), wakutana na Tume ya Katiba

Mwanachama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),  Subira Kibiga, akitoa maoni ya mtandao huo, kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo, Jumatano, Jan. 9, 2013, katika ofisi za tume jijini Dar es Salaam. Wengine ni wananchama wenzake  Diana Mwiru (kushoto) na Asseny Muro. (Picha zote na Ismail Ngayonga wa Tume ya Katiba)
Mwanachama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Asseny Muro, akitoa maoni ya mtandao huo, kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo, Jumatano, Jan. 9, 2013, Ofisi za tume jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa TGNP, Mary Rusimbi na Mjumbe wa Bodi ya mtandao huo, Profesa Ruth Meena.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, akiongea katika mkutano na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), uliolenga kupata maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya leo, Jumatano, Jan. 9, 2013, Ofisi za tume jijini Dar es Salaam. Katikati  ni Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao huo, Ussu Mallya na Mwenyekiti wa TGNP, Mary Rusimbi.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dk. Sengondo Mvungi, akiongea katika mkutano na viongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), uliolenga kupata maoni ya mtandao huo, kuhusu Katiba Mpya leo, Jumatano, Jan. 9, 2013, Ofisi za tume jijini Dar es Salaam. Katikati ni mjumbe wengine wa Tume Mary Kashonda na Salma Moulidi.
Baadhi ya Wajumbe ya Mabadiliko ya Katiba wakiwa katika picha ya pamoja na wanachama pamoja na viongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), mara baada ya mtandao huo, kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya leo, Jumatano, Jan. 9, 2013, Ofisi za tume jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment