
Rais Mahama alipokuwa anaapishwa mbele ya maelfu ya wananchi wa Ghana.
Chama rasmi cha upinzani nchini Ghana, kimesusia sherehe za kuapishwa kwa rais mpya John Mahama kufuatia uchaguzi wa mwezi jana uliokumbwa na utata.
Matokeo rasmi ya uchaguzi huo, yalionyesha bwana Mahama akiwa na aslimia 50.7 idadi ambayo inatosha kuweza kuzuia duru ya pili ya uchaguzi dhidi ya mpinzani wake Nana Akufo-Addo, aliyepata asilimia 47.7 ya kura.
Kabla ya kuapishwa kwake, bwana Mahama alitoa wito wa amani na umoja nchini Ghana, nchi ambayo inaonekana kama mfano mzuri wa demokrasia barani Afrika.
Bwana Mahama alikuwa makamu wa rais wa Ghana hadi pale kifo cha ghafla cha aliyekuwa rais,John Atta Mills kutokea mwezi Julai.
Tangu hapo alihudumu kama Rais wa mpito.

Rais John Mahama
Madai ya ulaghai na wizi wa kura, bila shaka yataathiri sifa yake kwa muda.
Lakini kuwepo kwa baadhi ya marais wa Afrika katika sherehe ya kuapishwa kwake, kunaonyesha kuwa bwana.
Mahama anaungwa mkono na jamii ya kimataifa.
Na sasa huenda mzozo huu ukatatuliwa kwa njia ya amani.

No comments:
Post a Comment