Katibu Mkiuu wa CCM Abdurahman Kinana akiwaaga wana CCM na wananchi waliojitokeza katika kituo kikuu cha Reli ya Kati na Sekretarieti nzima ya Chama cha Mapinduzi iliyooondoka leo kuelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya sherehe za miaka 36 ya CCM zinazotarajiwa kufanyika Februari 3 kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani humo mgeni rasmi akiwa, Dk. Jakaya Kikwete Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM. Baadhi ya Mablogger wameongozana na Sekretarieti hiyo, kwa ajili ya shughuli hiyo na zitakuwa habari za maadhimisho hayo, moja kwa moja kutoka mkoani Kigoma. Kulia ni Katibu wa Halmashauri, Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro.
Katibu wa Halmashauri Kuu na Ushirikiano wa Kimataifa Asha Rose Migiro akisalimiana na wana CCM waliojitokeza katika kuwaaga, kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam akiwaaga rasmi viongozi wa Sekretarieti ya CCM iliyoondoka leo kwa treni kwenda mkoani Kigoma.
Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akipanda treni akiwa ameongozana na viongozi wenzake.
Wana CCM wakishangilia wakati wakiwaaga viongozi wao walioondoka leo kwenda mkoani Kigoma
Wana CCM wakicheza muziki
Daniel Chongolo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano CCM akiweka sawa mambo kabla ya kuondoka .
Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na wana CCM kabla ya kuondoka katika kituo Kikuu cha Treni cha Reli ya Kati jijini Dar es salaam
Wana CCM na wananchi mbalimbali wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika kuwaaga viongozi wa Sekretarieti ya CCM leo. (Picha kwa hisani ya Fullshangwe)










No comments:
Post a Comment