TANGAZO


Friday, January 11, 2013

Rais wa Zanzibar, Dk. Shein azindua mradi wa 'One World Football for Africa'

 

 
Baadhi ya Watoto wakibeba mabango yenye ujumbe tofauti
 
unaosisitiza kulindwa haki zao, wakipita kwa maandamano mbele
 
ya Mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
 
Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein katika sherehe za uzinduzi wa
 
Mradi wa "ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA",
 
zilizofanyika leo, Uwanja wa Amaan Studiuam, ikiwa ni
 
shamrashamra za  maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi
 
 ya Zanzibar. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali
 
Mohamed Shein, akiwapungia mkono Vijana waliopita mbele ya
 
jukwaa la Uwanja wa Amaan, wakati akipokea maandamano ya
 
vijana katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa "ONE WORLD
 
FOOTBALL FOR AFRICA", ikiwa ni katika shamrashamra za
 
Miaka 49 ya maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kulia ni

Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na MIchezo Said Ali

Mbarouk
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali 
 
Mohamed Shein, akipokea kitabu kutoka kwa Nasra Sheikh
 
Mohamed wa Skuli ya Mwembeshauri, Mjini Unguja, kitabu 
 
chenye Agenda ya Watoto kuhusu usisitizaji kwa Serikali na Jamii
 
kushirikiana katika kuwapatia haki zao za Msingi bila
 
unyanyasaji, katika uzinduzi wa Mradi wa "ONE WORLD
 
FOOTBALL FOR AFRICA", Uwanja wa Amaan
 
ikiwa ni katika shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi
 
Matukufu ya Zanzibar. 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali

Mohamed Shein, akitia saini Mpira katika uzinduzi wa Mradi wa 

"ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA", mradi ambao

utawapatia vijana wa Zanzibar Mipira Ishirini Elfu (20,000), katika

vikundi mbalimbali na kupelekea kuongezeka kwa vipaji vya Soka

nchini, katika shamrashamra za kuadhimisha miaka 49 ya

Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali
 
Mohamed Shein, akimkabidhi tuzo mmoja wa wawakilishi wa
 
Mashirika yaliyosaidia kufanikisha mradi huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali
 
Mohamed Shein,akimkabidhi zawadi Mwakilishi wa Shirika la
 
UNICEF Paulo Edwards, katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa
 
ONE WORLD FOOTBALL FOR AFRICA", katika Uwanja wa
 
Amaan, ikiwa ni shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi
 
Matukufu ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment