TANGAZO


Monday, January 7, 2013

Rais Kikwete ahudhuria sherehe za kusimikwa wakfu Askofu Dk. Alex Seif Mkumbo wa KKKT Dayosisi ya Kati

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Gehaz Malasusa na Askofu  mpya wa KKKT, Dayosisi ya Kati, Dk. Alex Seif Mkumbo baada ya  sherehe ya Kusimikwa Wakfu askofu huyo katika Kanisa la Singida leo, Januari 6, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya kati, Dkt Alex Seif Mkumbo (mwenye fimbo), pamoja na viongozi wa Kanisa hilo, wakiongozwa na Askofu Mkuu, Dk. Alex Gehaz Malasusa (kulia kwa Rais), Msaidizi mpya wa Dayosisi hiyo, Mchungaji Syprian Yohana Hilinti (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Kone na viongozi wengine katika sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo, Januari 6, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na  Kiongozi wa Kanisa la KKKT nchini, Dk. Alex Gehaz Malasusa baada ya kupokea kamba kama ishara ya kupokea zawadi ya ngombe toka kwa Dayosisi hiyo, huku  Askofu  mpya wa KKKT, Dayosisi ya Kati Dk. Alex Seif Mkumbo, akishuhudia  katika sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo, Januari 6, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Kanisa la KKKT baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo, Januari 6, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na  Wasaidizi wa Maaskofu wa Kanisa la KKKT baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo Januari 6, 2013. (Picha zote na Ikulu)

No comments:

Post a Comment