TANGAZO


Friday, January 11, 2013

Matukio mbalimbali ya picha yahusuyo Mkutano wa Viongozi wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC leo jijini Dar es Salaam


Rais wa Serikali ya mpito ya Madagascar, Andry Rajoelina akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kupokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe leo, jijini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC-TROIKA), uliowahusisha Marais wa nchi za Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kutafuta suluhisho la migogoro ya nchi za Madagascar, Zimbabwe na machafuko nchini DRC.
(Picha zote na Aron Msigwa -MAELEZO).
Rais wa serikali ya mpito ya Madagascar Andry Rajoelina akikagua gwaride la maalum mara baada kuwasili jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete,  akimpokea Rais wa Serikali ya mpito ya Madagascar, Andry Rajoelina mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Wakuu wa nchi wanachama wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC-TROIKA), Rais wa Msumbiji Armando Guebuza (wa pili kushoto), Rais wa Namibia Hifikepunye Pohamba na Rais wa mpito wa Madagascar, Andry Rajoelina wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mkutano wa ndani kujadili mgogoro wa kikatiba wa Madagascar wakiongozwa na Mwenyekiti wa Asasi hiyo, Rais Jakaya Kikwete (wa pili kulia), Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Viongozi wakuu wa nchi zinaunda Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC – TROIKA, wakiwa kwenye picha ya pamoja. Kutoka kushoto Rais wa Namibia Hifikepunye Pohamba, Msumbiji Armando Guebuza, Mwenyekiti wa Asasi hiyo, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Rais wa Serikali ya mpito ya Madagascar, Andry Rajoelina aliyealikwa kwenye mkutano huo, kutafuta suluhu ya mgogoro wa nchi yake na Katibu Mkuu Mtendaji wa Asasi hiyo, Dk. Tomaz Salomao.
Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC-TROIKA), Rais Jakaya Kikwete akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kutoa mapendekezo yaliyofikiwa na viongozi wa nchi wananachama wa Asasi hiyo, kuhusiana na utafutaji wa suluhisho la kudumu la migogoro kwa nchi za Madagascar, Machafuko yanayoendelea DRC na hali ya Kisiasa nchini Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment