TANGAZO


Wednesday, January 2, 2013

Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) yawanoa Wahariri, Waandishi kuhusu Mifumo ya Hali ya Hewa, Utabiri na Lugha ya Utabiri, yawatunuku vyeti

Ofisa Mahusiano na Masoko wa TMA, Monica Mutoni, akiwasilisha mada kuhusu kazi za Mamlaka hiyo, Wadau wa TMA na Mrejesho, wakati wa warsha yao ya kuelemishwa kuhusu Mifumo ya Hali ya hewa, Utabiri na Lugha inayotumika katika utabiri, Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa, Ubungo Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


Msimamizi Mkuu wa Uchambuzi wa utabiri wa hali ya hewa, Wilberforce Kikwasi, akiwasilisha mada kuhusu utabiri wa muda mfupi na wa kati katika warsha hiyo.


Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Habari za Hali ya Hewa,  Helen Msemo, akiwasilisha mada kuhusu Utabiri wa muda mrefu katika warsha hiyo ya waandishi wa habari.


Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa katika warsha yao ya kuelemishwa kuhusu Mifumo ya Hali ya hewa, Utabiri na Lugha inayotumika katika utabiri, Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa, Ubungo Dar es Salaam leo.


Ofisa Mtabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Abubakar Lungo, akiwasilisha mada kuhusu utabiri wa muda mfupi na wa kati katika warsha hiyo.


Mchambuzi wa hali ya hewa, Agustino Nduganda, akiwasilisha utabiri wa hali ya hewa wa kesho katika warsha hiyo, pia kuelezea utabiri wa leo.


Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri, Dk. Hamza Kabelwa, akielezea kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa, kabla ya Mkurugenzi Mkuu, Agnes Kijazi (kushoto), hajaifungua warsha hiyo, jijini leo.



Mkurugunzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk. Agnes Kijazi, akizungumza wakati alipokuwa akiifungua warsha ya mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu Mifumo ya Hali ya hewa, Utabiri na Lugha inayotumika katika utabiri, Makao Makuu ya mamlaka hiyo, Ubungo Dar es Salaam leo.

Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugunzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk. Agnes Kijazi, wakati alipokuwa akiifungua warsha yao ya mafunzo kuhusu Mifumo ya Hali ya hewa, Utabiri na Lugha inayotumika katika utabiri, Makao Makuu ya mamlaka hiyo, Ubungo Dar es Salaam leo.

Mkurugunzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk. Agnes Kijazi, akimkabidhi Mhariri wa Radio Times, Adam, cheti cha kutambua ushiriki wake katika mafunzo hayo, wakati alipokuwa akiyafunga, Makao Makuu, Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.



 David Ramadhan wa Chanel Ten, akipokea cha kwake.


Mwafisi wa Majira, naye akichukua cha kwake kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi.


 Mhariri wa Habari wa gazeti la Uhuru, Ester Mvungi, akipatiwa cha kwake.

Fred Mwanjala wa Chanel ten, akikabidhiwa cheti chake na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dk. Agnes Kijazi.

Grace Ndosi wa gazeti la Majira naye akikabidhiwa cha kwake.

James wa Star Television akikabidhiwa cha kwake na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dk. Agnes Kijazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa blogu hii, Kassim Mbarouk, naye akishikishwa cha kwake na Mkurugunzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk. Agnes Kijazi, wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo, Makao Makuu, Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam. (Picha na Sleiman Mpochi)



Mbaraka Islam, akichukua cheti chake.


Anjumai wa gazeti la Uhuru, akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dk. Agnes Kijazi.








 Mhariri wa habari wa gazeti la Jambo Leo, Julian Msaky, akipokea cheti kutoka kwa Mkurugunzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk. Agnes Kijazi.





Mkurugunzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk. Agnes Kijazi, akiifunga warsha ya mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu Mifumo ya Hali ya hewa, Utabiri na Lugha inayotumika katika utabiri, Makao Makuu ya mamlaka hiyo, Ubungo Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa TMA, Dk. Hamza Kabelwa.

No comments:

Post a Comment