TANGAZO


Friday, January 25, 2013

Makamu wa Rais, Dk. Bilal awa mgeni rasmi maadhimisho ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, wakati alipowasili viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo, Januari 25, 2013, kwa ajili ya kuhudhuria mkesha wa sherehe za maadhimisho ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhamad (S.A.W)
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumin wa dini ya Kiislamu, katika mkesha wa  Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W), zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Kushoto kwake ni Sheikh Mohamed Ismail. 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, wakati akiwasili viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W.)
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh Mohamed Ismail, wakati akiondoka kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo, baada ya kuhudhuria sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W)
 
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akijumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W), yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Sheikh Mohamed Ismail, wakati alipokuwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo katika maadhimisho ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W)
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitoa salamu zake za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W), katika maadhimisho yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na waumin wa dini ya Kiislamu, wakijumuika pamoja katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W), zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR)

No comments:

Post a Comment