Silaha ambazo jeshi la Kenya lilinasa kutoka kwa Al
Shabaab
Serikali ya Kenya imeshutumu tishio la magaidi wa Al shabaab
walio nchini Somalia la kutaka kuwaua Wakenya wanaowazuilia iwapo matakwa yao
hayatasikilizwa na serikali hiyo.
Aidha imesema kuwa haiko tayari kwa mazungumzo yoyote na wapiganaji hao walio na uhusiano na kundi la Al Qaeeda.
Jeshi la Kenya limetaja vitisho hivyo kama kitendo cha kigaidi kwa kuwa waliotekwa ni wafanyakazi wa kutoa huduma za kimisaada na wala sio wanajeshi.
Al shabaab walitoa kanda ya video ya wakenya wawili waliowateka nyara mwaka mmoja uliopita na kusema kuwa watawaua ikiwa Kenya haitawaachilia wafungwa hao.
Wiki moja iliyopita wapiganaji hao walimuua jasusi mmoja wa Ufaransa Denis Allex kulipiza kisasi hatua ya Ufaransa kuwakandamiza waisilamu na kwa harakati zao za kijeshi nchini Mali.
Wapiganaji wa Al Shabaab wakiwa mazoezini
Alisema Serikali haiwezi kufanya mazungumzo na kundi la kigaidi. Kile ambacho Al Shabaab inafanya ni kitendo cha uhalifu ambacho kinapaswa kuadhibiwa .Alisema kuwa wanapaswa tu kuwaachilia.
Wawili hao walitekwa nyara mwezi Januari wakati wanamgambo walipovuka mpaka na kuingia Kenya na kisha kushambulia kituo cha polisi mjini Wajir huku polisi kadhaa wakiuawa kwenye shambulizi hilo.

No comments:
Post a Comment