TANGAZO


Thursday, January 24, 2013

Banc ABC yazindua tovuti itakayotoa habari za Ligi Kuu ya Vidacom

 
7
 
Ofisa Masoko wa Benc ABC, Evelyne Auguste akizindua mtandao wa http://www.ligikuu.co.tz/ , utakao toa habari za Ligi Kuu ya Vodacom, uliozinduliwa leo, Hoteli ya JB Belmonte, jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia katika picha wanaoshuhudia tukio hilo, ni Rodney Rugambo, Meneja Masoko wa Push Mobale, Wawila Nzowa, Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Lajann E Systems na kushoto ni Dennis Rauya, Meneja wa BencABC, tawi la Quality Centre jijini Dar es Salaam na Salum Mwalimu, Meneja Mawasiliano wa Vodacom.
6
 
Kutoka kulia ni Rodney Rugambo, Wawila Nzowa, Evelyne Auguste na Dennis Rauya wakifuatilia maelezo ya mmoja wa wataalam wa mtandao huo, wakati wa uzinduzi wake.
1 
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika uzinduzi wa mtandao huo.
2
 
Ofisa Masoko wa Benc ABC, Evelyne Auguste akitoa maelezo juu ya udhamini wa benki hiyo, kwa mtandao wa Ligi Kuu.
3Rodney Rugambo, Meneja Masoko wa Push Mobile, akizungumzia kuhusu udhamini wa kampuni hiyo kwa mtandao huo ili kuboresha mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini .

4
Meneja Mawasiliano wa Vodacom, Salim Mwalim akiishukuru Kampuni hiyo kwa kuanzisha mtandao huo, ambao amesema utasaidia sana kutangaza mpira wa miguu nje ya nchi na kuwatangaza wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom. (Picha zote na mpigapicha wetu)

No comments:

Post a Comment