Familia zilizoathiriwa kwa mujibu wa Gazeti la Standard Nchini
Kenya wakipekuwa mali yao baada ya maporomoko hayo ya Ardhi.
Watu wanane wamekufa baada ya nyumba kadha kufukiwa na
maporomoko ya ardhi katika eneo la bonde la Kerio, magharibi mwa Kenya, jana
usiku.
Chama cha Msalaba Mwekundu cha Kenya kinasaidia jitihada za uokoaji na kutoa taarifa kwamba miili miili ya watu wanane imeonekana na watu wengine watano waliokolewa mapema leo.
Watu wengi hawana makaazi kutokana na nyumba zao kusombwa na maji au kufukiwa na maporomoko ya ardhi.

No comments:
Post a Comment