TANGAZO


Thursday, November 22, 2012

Naibu Waziri Makamba aufungua Mkutano wa 21 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, akisaini kitabu cha wageni wakati alipofika kuufungua mkutano wa 21 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, Dar es Salaam leo asubuhi. Katikati ni Postamasta Mkuu, Deos Mndeme na kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa wizara hiyo, Eng. Cralence Ichwekeleza. (Picha zote na Kassim Mbarouk)


Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Deos Mndeme, akizungumza wakati wa mkutano huo wa 21 wa Baraza la Wafanyakazi wa shirika hilo leo. Kulia ni mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba na wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo, Dk. Yamungu Kayandabila.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo, Dk. Yamungu Kayandabila, akizunguma katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (wa pili kulia), kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa baraza hilo. 


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakati alipokuwa akiufungua mkutano wa 21 wa baraza hilo jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo, Dk. Yamungu Kayandabila na katikati ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Emmanuel Lugomela.


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo, wakati alipokuwa akiufungua mkutano wa 21 wa baraza hilo jijini leo.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, wakati alipokuwa akiufungua mkutano wa 21 wa baraza hilo jijini leo.



Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Emmanuel Lugomela, akizungumza wakati alipokuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu baraza hilo na Shirika kwa ujumla. Kulia ni mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo, Dk. Yamungu Kayandabila.


Mjumbe wa Baraza hilo la Wafanyakazi kutoka Morogoro, Midred Achimpota, akitoa neno la shukurani kwa mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (wa pili kulia), kutokana na hotuba yake aliyoitoa katika ufunguzi huo. Kulia ni Postamasta Mkuu, Deos Mndeme.



Baadhi ya waandishi wa habari na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, wakati alipokuwa akiufungua mkutano wa 21 wa baraza hilo jijini leo.


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (katikati waliokaa mbele),  akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, mara baada ya kuufungua mkutano wa 21 wa baraza hilo, Dar es Salaam leo.


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (kulia),  akisalimiana na kuagana na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, mara baada ya kuufungua mkutano wao wa  21 wa baraza hilo, jijini leo.



Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (kushoto),  akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kuufungua mkutano wa 21 wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment