TANGAZO


Friday, November 23, 2012

Matukio mbalimbali ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Shein, alipotua nchini Vietnam na muendelezo wa ziara yake nchini Hhmo


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed shein na mkewe, mama Mwanamwema Shein, wakipokea mashada ya maua kama ishara ya ukaribisho katika Ikulu ya Vietnam, alipofika kwa mazungumzo na Makamo wa Rais wa Vietnam, Bibi Nguyen Thi Doan, akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya wiki moja ya  Kiserikali nchini humo.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed shein, akiwatambulisha viongozi aliofuatana nao kwa Makamo wa Rais wa Vietnam, Bibi Nguyen Thi Doan, walipowasili Ikulu ya nchi hiyo kwa mazungumzo ya kuimarisha uhusiano na Ushirikiano baina ya pande zote, akiwa katika ziara rasmi ya wiki moja nchini humo.
 
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Makamo wa Rais wa Vietnam, Bibi Nguyen Thi Doan, alipowasili Ikulu nchini Vietnam, akifuatana na mumuwe, Rais wa Zanzibar katika ziara rasmi ya wiki moja ya Kiserikali chini Vietnam.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed shein, akisalimiana na Mawaziri na viongozi mbalimbali wa nchini Vietnam alipofika Ikulu ya nchi hiyo, kwa mazungumzo na Makamo wa Rais wa Vietnam, Bibi Nguyen Thi Doan, akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed shein, akisalimiana na Makamo wa Rais wa Vietnam, Bibi Nguyen Thi Doan, alipowasili Ikulu nchini Vietnam, akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed shein (katikati), akiwa ujumbe aliofuatana nao katika Mkutano maalum na Uongozi wa Serikali ya Vietnam, ukiongozwa na Makamo wa Rais wa nchi hiyo, Bibi Nguyen Thi Doan (hawapo pichani), katika ukumbi wa Ikulu, kuimarisha Uhusiano na Ushirikiano baina ya pande mbili hizo, katika ziara rasmi ya Kiserikali ya wiki moja.
 
Viongozi wa Serikali waliofuatana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Dk. Ali Mohamed Shein, wakiwa kwenye mkutano maalum na uongozi wa Serikali ya Vietnam.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiteta jambo na mwenyeji wake, Kiongozi Mkuu katika Ofisi ya Rais Ikulu nchini Vietnam, Giang Son, wakiwa katika ukumbi wa Mapunziko (VIP) katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hanoi nchini Vietnam, akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali jana.
 
Mama Mwanamwema Shein (kulia), Waziri wa Kazi Uwezeshaji wananchi kiuchumi na Ushirika, Haroun Ali Suleiman (katikati) na Balozi wa Tanzania nchini China pia akiwa anafanyakazi zake nchini Vietnam, Philip Marmo, wakiwa katika chumba cha mapumziko (VIP) katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hanoi, nchini Vietnam, wakiwa ni miongoni mwa ujumbe wa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein nchini Vietnam.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Maofisa wa Serikali ya Vietnam, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hanoi, nchini Vietnam, akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali ya wiki moja nchini humo.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), akifuatana na mwenyeji wake, Kiongozi Mkuu katika Ofisi ya Rais Ikulu Nchini Vietnam,  Giang Son (wa pili kushoto), baada ya mapokezi rasmi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hanoi, nchini Vietnam, akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali ya wiki moja nchini humo jana. Kushoto ni Balozi wa Tanzania, nchini China ambaye pia anawakililisha nchini Vietnam, Philip Marmo. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)

No comments:

Post a Comment