TANGAZO


Saturday, October 27, 2012

Waislamu wengi wauwawa Burma

Wilaya nzima inayokaliwa na Waislamu waitwao Rohingya imeangamizwa katika ghasia za karibuni kabisa za kidini magharibi mwa Burma.

 
Warohingya wakiwa kwenye makambi

Shirika la kutetea haki za kibinaadamu, Human Rights Watch, limechapisha picha zilizopigwa na satalaiti, ambazo zinaonesha kuwa nyumba zaidi ya 800 zimechomwa moto kwenye mji wa kando ya bahari uitwao Kyaukpyu.
Wakuu wamesema kuwa Waislamu zaidi ya 3000 wamenasa kwenye kisiwa baada ya kukimbia makwao kwa mashua, na wamekataliwa kuingia katika mji mkuu wa jimbo, Sittwe.
Serikali ya Burma inasema kuwa watu zaidi ya 60 waliuwawa katika juma la mapigano baina ya Waislamu na Wa-Buddha katika jimbo la Rakhine, na kuna wasiwasi kuwa idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi.
Waislamu hao hawatambuliwi kuwa raia wa Burma.

No comments:

Post a Comment