TANGAZO


Wednesday, October 24, 2012

Utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Kilombero mkoani Morogoro wafanyika jijini Dar es Salaam

Mtendaji Mkuu wa Tanroad, Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) na  Mtendaji Mkuu kutoka Kampuni ya Ujenzi ya China Railway 15 Bureau Group Corporation (CR15G), Zhang Tonggang (kulia) wakitia saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Kilombero lenye urefu wa  meta 384 na ujenzi wa barabara zake za miingilio za lami (kilometa 9.142) pamoja na ujenzi wake utagharimu shilingi bilioni 53.2. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Ujenzi, Dk.  John Magufuli (katikati nyuma waliosimama) na kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Herbert Mrango. Pichani kutoka kushoto ni  Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Tanroads, Bibi Hawa Mmanga, Mbunge wa Mikumi, Abdul Salim Ameir na Mbunge kutoka Morogoro Kusini Innocent Kalgeris. (Picha na Mwanakombo jumaa- MAELEZO)
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi ya China  Railway  15 Bureau Group Corporation (CR15G), Bw. Zhang Tonggang, wakibadilishana hati baada ya kutia saini kwa ajili ya ujenzi wa dara la Kilombero, mkoani Morogoro. Daraja hilo, lenye urefu wa kilometa 384 litagharimu shilingi bilioni 53.2. Ujenzi wa daraja hilo utaziunganisha Wilaya za Mahenge na Ulanga pamoja na kuboresha usafiri wa Mikoa ya Kusini  na kuleta kichocheo cha ukuaji wa shughuli za kiuchumi. 
Waziri John Magufuli akisisistita jambo wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Mramgo ni kushoto ni Mbunge wa Morogoro  Kusini, Innocent Kalgeris.

No comments:

Post a Comment