TANGAZO


Tuesday, October 16, 2012

Sultan Qaboos amtunuku Rais Kikwete Nishani ya Juu ya Heshima


Sultani wa Oman, Al-Qaboos bin Said Al Said (kulia), akimtunuku Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Nishani ya Juu ya Heshima ya Taifa la Oman, wakati wa dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake jana jioni katika kasri ya  AL Alam, jijini Muscat Oman.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi zawadi mwenyeji wake, Sultani wa Oman Al-Qaboos bin Said Al Said katika kasri ya AL Alam, jijini Muscat Oman jana jioni muda mfupi kabla ya dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa kwa heshima yake.

Sultan Al-Qaboos bin Said Al Said, akimpongeza Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumtunuku Nishani ya Juu ya Heshima ya Taifa la Oman, jana jioni katika kasri ya AL Alam, jijini Muscat Oman jana jioni. Rais Kikwete aliwasili nchini Oman jana jioni kwa ziara rasmi ya siku tatu. (Picha zote na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment