Emmanuel Okwi wa Simba akimtoka Temi Felix wa Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
Amir Maftah wa Simba akimtoka Temi Felix wa Kagera Sugar, wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.
.
Amir Maftah wa Simba (kulia), akipambana na Amandus Nesta wa Kagera Sugar, wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Emmanuel Okwi wa Simba (kushoto), akimpongeza Felix Sunzu baada ya kufanikiwa kuifungia timu yao, goli la kwanza dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mchezaji Wilfred Ammeh wa Kagera Sugar (kulia), akipiga mpira mbele ya Amri Kiemba wa Simba, wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo na kugawana pointi baada ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo huo. Katikati ni Mrisho Ngassa wa Simba.
Emmanuel Okwi wa Simba, akijaribu kumpiga chenga Malegesi Mwangwa (kushoto), wa Kagera Sugar.
Nassor Masoud 'Chollo', akitolewa nje baada ya kupasuka juu ya jicho katika mchezo huo leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Nassor Masoud 'Chollo', (kushoto), akikimbilia mpira na Malegesi Mwangwa wa Kagera Sugar katika mchezo huo, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo huo, wakati timu yao ikiongoza kwa mabao 2 kabla ya Kagera Sugar kusawazisha mabao hayo.
Hadi kipenga cha mwisho katika mchezo huo, kibao cha matokeo kilikuwa kikionesha Simba 2 na Kagera Sugar 2.
No comments:
Post a Comment