Mwenyekiti
wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC), Fatuma Riyami (kulia), akizungumza na
waandishi wa
habari leo, jijini Dar es Salaam, kuhusu Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Wanawake
Wafanyabiashara wa Nchi za Mashariki mwa Afrika, unaofanyika Tanzania kwa mara
ya kwanza. Mkutano huo unaotarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk.
Mohamed Gharib Bilal.
Kushoto ni Makamu wa Mwenyekiti wa TWCC Anna Matinde. Mkutano huo unafunguliwa
kesho Jumatau katika Hotel Kunduchi Beach.
|
Mwenyekiti wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC), Fatuma Riyami (kulia), akizungumza na waandishiwa habari leo, kuhusu Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Wanawake Wafanyabiashara wa Nchi za Mashariki mwa Afrika, unaofanyika Tanzania kwa mara ya kwanza. Kushoto ni Makamu wa Mwenyekiti wa TWCC Anna Matinde. Mkutano huo unafunguliwa kesho Jumatau katika Hotel Kunduchi Beach. (Picha zote na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es Salaam)
Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es Salaam
21.10.2012
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib
Bilal anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa
Kimataifa wa Wanawake wafanyabiashara wa Nchi za Mashariki mwa Afrika unaonza
kesho, jijini Dar es salaam kwa lengo la kuimarisha mtandao
wao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa
Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Fatma Riyami wakati
akiongea na waandishi wa habari Ofisi
kwake.
Amesema kuwa Mkutano huo ambao ni wa saba(7)
unafanyika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza tangu walipoanzisha ushirikiano
huo wa wanawake wafanyabiashara kwa nchi za Afrika Mashariki.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa wajumbe wa Mkutano
huo wanatarajiwa kutoka katika Nchi za Kenya, Uganda, Rwanda , Burundi, Ethiopia
, Sudan Kusini na mwenyeji Tanzania.
Amesema kuwa Mkutano huo utakuwa
fursa nzuri kwa wajumbe kutoka nchi zote saba kubadilishana uzoefu katika kazi
ya kuwainua kiuchumi wakimama na kuimarisha Mtandao wa Wafanyabiashara wanawake
katika Nchi za Afrika Mashariki.
Ameongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kufanya soko
la wafanyabiasha wanawake wa Afrika Mashariki kuwa kubwa na hivyo kuwainua
kiuchumi wakimama.
Aidha Bibi Fatma Riyami amesema kuwa TWCC
imeanzisha matawi katika Mikoa ya Kagera, Mwanza, Pwani, Dodoma, Mbeya, Dar es
salaam na Arusha ikiwa na lengo la kutaka kuwa karibu na wafanfanyabiashara
wanawake kwa nia kuimarisha Umoja wao.
Wakati huo Mwenyekiti huyo amewasisitiza wajumbe
wa Mkutano huo kufika katika Hoteli hiyo ifikapo saa 1.30 Asubuhi , Mgeni rasmi
atafungua mkutano huo saa 2.00 kamili |
No comments:
Post a Comment