Wanajeshi wa Sudan Kusini
Ripoti ya Shirika la Amnesty International imefichua kuwa
Wanajeshi wa Sudan Kusini wanaoendeleza zoezi la kuwapokonya wenyeji silaha
haramu mashariki mwa nchi hiyo, wanatumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia.
Serikali ilizindua zoezi hilo katika juhudi za kurudisha amani mapema mwaka huu kufuatia mapigano ya kikabila yaliyozuka katika Jimbo la Jonglei ambako mamia ya watu waliuawa.
Hata hivyo, visa vya mateso na unyanyasaji vimeripotiwa kutoka kwa Wanajeshi na Polisi wanaosaka Silaha haramu zinazotumika kwenye mapigano hayo.
Mwandishi wa BBC amesema kwamba hapo awali Serikali ilipuuza tetesi kuhusiana na visa hivyo vya mateso na unyanyasaji tangu Taifa changa la Sudan Kusini lilipojinyakulia uhuru wake zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

No comments:
Post a Comment