TANGAZO


Saturday, October 20, 2012

Makamu wa Rais Dk. Bilal afungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), mjini Dodoma leo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati alipokuwa akiufungua mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), uliofanyika leo Oktoba 20, 2012 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango, mjini Dodoma, sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT, Taifa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma leo, Oktoba 20, 2012 kwa ajili ya kuufungua mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT),  uliofanyika sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT, Taifa. Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa nne wa UWT, Taifa wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka kwenye mkutano huo leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania, (UWT) Taifa, anayemaliza muda wake, Sophia Simba, wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), uliofanyika leo Oktoba 20, 2012, sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Taifa.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania, (UWT) Taifa, anayemaliza muda wake, Sophia Simba, (katikati) na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), uliofanyika leo, Oktoba 20, 2012, sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Taifa. Baadhi ya wake wa Viongozi, wakiwa ukumbini humo wakati wa ufunguzi huo wa mkutano Mkuu wa  Nane wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), uliofanyika leo Oktoba 20, 2012, sambamba na uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Taifa.Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Nane wa UWT, waliohudhuria mkutano huo leo katika Chuo cha Mipango mjini Dodoma.


No comments:

Post a Comment