TANGAZO


Thursday, October 25, 2012

Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Arusha alipuliwa kwa bomu anusurika kufa

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akiingia Hospitali kwenda kumjulia hali Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha  Abdulkadir Jonjo, hospitalini leo.


Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha  Abdulkadir Jonjo akiwa amelazwa Hospitali ya Mount Meru baada ya kulipuliwa kwa bomu nyumbani kwake.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa  Mulongo akimjulia hali Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha  Abdulkadir Jonjo, Hospitali ya Mount Meru leo.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa  Mulongo, akimjulia hali Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha  Abdulkadir Jonjo, hospitalini leo, huku akihojiwa na waandishi wa habari Hospitali ya Mount Meru leo.



Waandishi wa habari wakichukua habari za Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha  Abdulkadir Jonjo, Hospitali ya Mount Meru leo.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas, akizungumza na waandishi wa habari, kuelezea tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas, akiangalia masalia ya bomu lililomlipua Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Arusha, Abdulkadir Jonjo.



Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), wataalamu wa mabomu, wakiangalia sehemu liliporushwa bomu na kuangalia kama lipo lingine ambalo halijalipuka.


Baadhi ya vifaa vilivyoharaibiwa na bomu hilo nyumbani kwa Katibu wa Bakwata, Mkowa wa Arusha.

Na Mery Kitosio,ARUSHA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida katibu wa Bakwata mkoa wa Arusha ,
Abdulkarimu Jonjo amenusurika kufa mara baada ya kulipukiwa na kitu
kinachosadikiwa kuwa ni boma wakati akiwa amelala nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo, majira ya saa 6:30 usiku eneo la Esso jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kamati ya usalama
inayoongozwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa  Mulongo huku akiwa
amelazwa katika hospitali ya mount Meru wodi ya majeruhi, Jonjo alisema kuwa, alisema kuwa majira ya saa 6 ;30 usiku alisikia kishindo kikubwa sana dirishani kwake akiwa amelala ndipo alipoamka.

Alisema kuwa, mara baada ya kuamka aliona kitu kinachowaka kama mshumaa ambapo alijaribu kukisogelea kwa lengo la kukishika na kukichunguza ndipo ghafla kilipolipuka na na kumrusha mbali , na baada ya muda kidogo aliamka na kwenda kuomba msaada kwa majirani.

‘Kitu hicho kilinishtua sana kwani sikutarajia na mara kilipolipuka kilinisababishia nipate maumivu makali sana na mara baada ya kukaa chini kwa muda mfupi ndipo nilifaniukiwa kunyanyuka na kuomba msaada kwa majirani ambao walifanikiwa kunisaidia nna kuniwaisha hospitalini hadi mnavyoniona hapa sasa hivi , hali yangu ni nzuri na namshukuru mungu’alisema Jonjo.

Alisema kuwa, tukio hilo linamtatanisha kwani hajaweza kujua chanzo
cha tukio hadi sasa hivi na anaiomba serikali iweze kufanya  uchunguzi
wa haraka kwani tukio hilo linaatarisha maisha ya watu wengi kwani ni
la kutisha sana .

Akingumzia tukio hilo, Mkuu wa mkoa wa Arusha mara baada ya kutembelea
hospitalini na nyumbani  kwake, alisema kuwa , tukio hilo  lina utata
mkubwa na linahitaji uchunguzi mkubwa na wa haraka kwani ni tukio
ambalo linasikitisha sana na limebugikwa na utata mkubwa sana.

Mulongo alisema kuwa tukio hilo linahitaji kupewa uzito mkubwa sana ndio maana askari wa jeshi la wananchi wamefika eneo la tukio ili kufanya upelelezi wa haraka na kina hivyo hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa kwa haraka kwa waliohusika na tukio hilo ambalo linaatarisha maisha ya watu.

‘Ninaombeni wananchi wa Arusha wavute subiri na wasiwe na wasiwasi katika kipindi hiki ambacho tunafanya buchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hili na ninaombeni sana lisihusishwe na maswala ni kidini , hii mapema sana kuweza kugundua chanzo cha tukio hilo na kama mtalihusisha tukio hili na maswala ya dini basi mtazua mambo mengine ambayo yatakuwa makubwa zaidi ya hayo hivyo naombeni mtupe nafasi tufanye uchunguzi wa kina’alisema Mulongo.

Katika hatua nyingine , Mganga mfawidhi wa hopitali ya mkoa ya Mount Meru, Dkt Ijosia Mlay alidhinitisha kupomkea katibu huyo akiwa katika hali ya maumivu sana ambapo jitihada mbalimbali za kitabibu zilifanyika ili kuweza kuokoa maisha yake  na hadi sasa anaendelea vizuri.

Alisema kuwa, katibu huyo amepata majeraha sehemu  mbalimbali za mwili
wake hasa katika maeneo ya usoni, kichwani, kifuani na mkono wa kulia
ambapo alikuwa akitokwa na damu usoni na kuumia mkono wa kulia.

Dkt Mlaya alisema kuwa,maumivu hayo yalitokana na kitu kinachosadikiwa na kuwa ni baruti ambayo iliwekwa mfumo wa bomu na ilipolipuka ilimsababishia  majeraha hayo na kwa sasa hivi anaendelea vizuri na ameweza kujitambua huku akiendelea  kupewa matibabu hospitalini hapo.

Hata hivyo kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema uchunguzi unaedelea katika kuwabaini waliohusika na tukio hilo.

Awali tukio hilo limetokea siku chache tu , mara baada ya katibu huyo kutoa tamko dhidi ya vijana wanne wa dini ya kiislamu waliotekwa na watu wasijulikana na kuvuliwa nguo zote huku wakipata mateso makali sana kutokana na kile kichodaiwa kuwa vijana hao wanaunga mkono kuwepo kwa katibu huyo kuendelea kuongoza BAKWATA mkoa wa Arusha huku  kundi lingine likipinga hatua ya kuwepo kwa katibu huyo.

No comments:

Post a Comment