Wapiganaji wa kiisilamu wa kundi la Al Shabaab wamepiga marufuku shirika la mwisho la misaada lililosalia kufanya kazi katika maeneo wanayodhibiti.
Al-Shabaab imetuhumu shirika hilo la Uingereza, Islamic Relief, kwa kuendesha shughuli zake kwa niaba ya shirika la mpango wa chakula duniani WHO ambalo limepigwa marufuku katika maeneo hayo.
Islamic Relief limekanusha madai hayo na kuomba liruhusiwe kuendesha shughuli zake.
Shirika hilo linatoa chakula , maji na huduma za afya kwa zaidi ya watu milioni moja nchini Somalia.
Al Shabaab lingali linadhibiti maeneo ya vijijii na Kusini mwa Somalia licha ya kufurushwa kutoka miji mikubwa ya Somalia.
No comments:
Post a Comment