WASANII Lucas Mkenda ‘Mr Nice’, Seif Shabani ‘Matonya’, Ally Mohamed ‘Z-Anto’, Bi. Mwanahawa Ally wa East African Melody, Kundi la Ngoma za Asili la Nakalandima na Kundi la New Zanzibar Stars Modern Taarab usiku wa kuamkia leo wamefunika vilivyo katika Usiku wa Fleva za Dhahabu uliofanyika kwenye ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam, kama inavyoonekana katika matukio tofauti pichani.
Mkali wa Bongo Fleva, Seif Shabani ‘Matonya’
akipagawisha katika Usiku wa Fleva za Dhahabu ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia
leo.
Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ akifanya makamuzi katika Usiku wa
Fleva za Dhahabu uliofanyika Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Ally Mohamed ‘Z-Anto’ akiwarusha mashabiki
waliohudhuria ndani ya Dar Live.
Msanii wa muziki wa Tarab, Bi. Mwanahawa Ally wa East African Melody, akitumbuiza katika Usiku
wa Fleva za Dhahabu uliofanyika Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Kundi la New Zanzibar Stars Modern Taarab, likiwapagawisha
mashabiki.
Kundi la ngoma za asili la Nokalandima likionyesha makali
yake.
Mwanasarakasi Lwiti Nzoa akionesha
ufundi wake katika mambo ya sarakasi.
Lwiti Nzoa, akizidi kuonyesha mbwembwe zake.
Matonya akiimba Wimbo wa Vaileth uliompagawisha shabiki wake.
Msanii Luca Mkenda 'Mr Nice', akizidi kuwapa raha mashabiki.
Msanii Z- Anto na kundi lake wakifanya mambo.
Msanii Zahir Hamis wa kundi la New Zanzibar Stars Modern Taarab,
akiwarusha roho mashabiki wa kundi hilo katika onesho hilo.
Msanii wa Kundi la Ngoma za Asili la Nokalandima
akipagawisha.
No comments:
Post a Comment