TANGAZO


Saturday, September 29, 2012

Boko Haram wamo jeshini piya

Jeshi la Nigeria linasema kuwa askari wa usalama wamekamatwa wakishukiwa kuwa na uhusiano na kundi la Kiislamu la wapiganaji, Boko Haram.

Silaha za Boko haram zilizogundulikana mwezi Agosti
Msemaji wa jeshi, Kanali Sagir Musa, aliiambia BBC kwamba watu kadha wamekamatwa kaskazini mwa nchi katika majimbo ya Borno na Yobe.
Alisema afisa wa uhamiaji aliyekamatwa mwezi uliopita, aliwasaidia kuwatambua askari wa usalama wenye uhusiano na wapiganaji.
Wadadisi waliwahi kudokeza kuwa vita dhidi ya Boko Haram havifanikiwi kwa sababu wapiganaji hao wamo jeshini.

No comments:

Post a Comment