TANGAZO


Tuesday, August 14, 2012

Stars yawasili Gaborone kukipiga na Zebras

 Wachezaji wa Taifa stars wakiwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Gaborone, Botswana  leo, kwa ajili ya kukipiga na timu ya Taifa ya nchi hiyo, Zebras kesho.
Wachezaji wa Taifa Stars wakitoka kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Gaborone, Botswana mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kukipiga na timu ya Taifa ya nchi hiyo, Zebras kesho.
Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa na mizigo yao, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Gaborone, Botswana mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kukipiga na timu ya Taifa ya nchi hiyo, Zebras kesho.
Baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars wakitoka kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Gaborone, Botswana mara baada ya kuwasili uwanjani hapo leo.
Badhi ya wachezaji wa Taifa Stars wakiwa uwanjani hapo mara baada ya kuwasili nchini humo leo asubuhi kwa ajili ya pambano lao na timu ya Taifa ya nchi hiyo, Zebras kesho. (Picha zote na habari na mdau wetu)
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kikiwa na wachezaji 17 kimewasili leo asubuhi jijini Gaborone tayari kwa mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya wenyeji Botswana 'Zebras' itakayochezwa kesho (Agosti 15 mwaka huu).
Stars imetua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama saa 5.45 leo asubuhi kwa saa za hapa
ambapo nyumbani ni 6.45 na kupokewa na viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Botswana (BFA) na
Watanzania wanaoishi hapa Botswana.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura baadhi ya wachezaji walioko kwenye kikosi hicho ni Frank Domayo, Ramadhan Singano na Simon Msuva
ambao walijiunga na Stars saa chache baada ya kurejea kutoka Nigeria ambapo walikuwa na timu ya vijana
wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) ambayo Jumapili ilicheza mechi ya mashindano ya Afrika
dhidi ya Nigeria (Flying Eagles).
Wachezaji wengine kwenye kikosi kilichoko Botswana ni Aggrey Morris, Amir Maftah, Athuman Idd, Erasto
Nyoni, Haruna Moshi, Juma Kaseja, Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa, Mwadini Ally, Mwinyi Kazimoto,
Ramadhan Chombo, Salum Abubakar, Said Bahanuzi na Shabani Nditi.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia kwenye hoteli ya Oasis ambayo pia ndipo
Zebras imepiga kambi kwa ajili ya mechi hiyo. Mechi itaanza kesho saa 1 kamili usiku kwa saa za hapa na
itafanyika kwenye Uwanja wa Molepolole Sports Complex. Uwanja wa Taifa wa Botswana hivi sasa uko
kwenye matengenezo.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema mechi hiyo ni muhimu kwa vile timu yake bado
inakabiliwa na mechi za Kombe la Dunia Kanda ya Afrika, na michuano ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji
wa Ndani (CHAN) inayotarajia kuanza baadaye mwaka huu.

No comments:

Post a Comment