TANGAZO


Thursday, August 9, 2012

Azam yakubali 2-0 nyumbani kwao mbele ya Mtibwa Sugar

 Shaaban Kisiga wa Mtibwa Sugar (kushoto) na Hussein Javu, wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ya Super 8, uliochezwa Uwanja wa Chamazi, unaomilikiwa na Azam. Ligi inayocdhaminiwa na BacABC. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Wachezaji wa Mtibwa wakiswali kushukuru na kushangilia goli la kwanza la timu hiyo dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam. Mtibwa ilishinda mabao 2-0 katika mchezo huo wa Ligi ya Super 8, inayodhaminiwa na BacABC.

Wachezaji wa Mtibwa wakipongezana baada ya Shaaban Kisiga kuipatia  timu hiyo goli la kwanza dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam, katika mchezo huo wa Ligi ya Super 8, inayodhaminiwa na BacABC.

Mchezaji Abdul Kassim 'Babii wa Azam FC, akiruka juu kuuwahi mpira uliokuwa ukiwaniwa na Hussein Javu (wa pili kushoto), wakati wa mchezo huo.

 Said Morad wa Azam FC, akilala chini kuuondoa mpira miguuni mwa Jamal Mnyate  wa Mtibwa Sugar katika mchezo huo. 

 Mshambuliaji wa Azam FC, akijaribu kumpiga chenga Babuu Ally Seif wa Mtibwa.

 Mchezaji wa Azam FC, akilala chini kuuondoa mpira miguuni mwa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar.

Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Shaaban Kisiga (kulia), akimtoka golikipa wa Azam FC (aliyelala chini), baada ya kumpiga chenga na kufunga moja ya magoli ya timu hiyo.

Mchezaji Jamal Mnyate wa Mtibwa akitafuta mbinu ya kumpita Abdulhalim Humud wa Azam FC, wakati wa mchezo huo wa Sper 8, uliochezwa Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam leo jioni ambapo Mtibwa ilishinda mabao 2-0.
Mashabiki wachache waliohudhuria kuangalia mchezo huo, wakifuatilia kwa makini matukio ya uwanjani kati ya wachezaji wa timu hizo walipokuwa wakipambana kuusaka ushindi.

No comments:

Post a Comment