TANGAZO


Saturday, July 14, 2012

Ufunguzi mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akilakiwa na wanachama  wakati alipowasili Makao Makuu ya Chama hicho, Buguruni jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Julai 14, 2012 kwa ajili ya kuufungua mkutano wa siku mbili wa Baraza Kuu la Uongozi. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF), wakimpokea Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, wakati alipokuwa akiingia kwenye ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya CUF kwa ajili ya kuufungua mkutano wa baraza hilo leo.
  
 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Bara, Julias Mtatiro, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho leo, Julai 14, 2014. Katikati ni Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba na kulia ni Makamu Mwenyekiti, Machano Khamis Ali.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF), wakiangalia makabrasha yao kabla ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, kuufungua mkutano wao, Makao Makuu ya Chama hicho, Buguruni Dar es Salaam leo.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF), wakiangalia makabrasha yao kabla ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, kuufungua rasmi mkutano wao, Makao Makuu ya Chama hicho, Buguruni Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wakati alipokuwa akiifungua mkutano wa baraza hilo, Makao Makuu ya Chama hicho, Buguruni jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Julai 14, 2012. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu CUF Bara, Julias Mtatiro.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wakati wa mkutano wao, Makao Makuu ya Chama hicho, Buguruni jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Julai 14, 2012. Katikati ni Makamu Mwenyekiti, Machano Khamis Ali na kulia ni Naibu Katibu Mkuu CUF Visiwani, Ismail Jussa Ladhu.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na Wajumbe wa Baraza hilo, wakati akiufungua mkutano wao wa Baraza Kuu la Uongozi, Makao Makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Julai 14, 2012. Kulia ni Makamu Mwenyekiti, Machano Khamis Ali.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF), wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, wakati alipokuwa akiufungua mkutano wao wa siku mbili, Makao Makuu ya Chama hicho, Buguruni Dar es Salaam leo.

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, jijini Dar es Salaam, wakiandika kutoka kwenye hotuba ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, wakati akiufungua mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi, Makao Makuu ya Chama hicho, Buguruni Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment