Mchezaji wa timu ya Twiga Stars Mawanahamisi Omary akiondoka na mpira kuelekea goli la timu ya wanawake ya Ethiopia huku mabeki wa timu hiyo wakiwania mpira huo katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwaka ujao, mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa Taifa wa Dar es salaam jioni hii.
Mpira umemalizika na Twiga Stars kukubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya timu hiyo ya Ethiopia, ushindi uliowatoa Twiga Stars nje mashindano hayo.
Marefa wakiziongoza timu za Ethiopia na Twiga Stars ya Tanzania, kuingia uwanjani kwa mpambano huo leo jioni.
Wachezaji wa timu za wanawake wa Tanzania na Ethiopia wakiingia uwanjani tayari kwa kuanza mchezo huo.
Wachezaji wa Twiga Stars na Ethiopia wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Mashabiki wakiwa kwenye jukwaa kuu la Uwanja wa Taifa, kuangalia mpambano kati ya Twiga Stars na Ethiopia leo. (Picha na Fullshangwe blogspot)
Kikosi cha Stars. (Picha na Mpiga Picha wa Habari Mseto Blog)
Kikosi cha Ethipoia
Mshambuliaji wa timu ya Soka ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’, Mwanahamisi Omari akichuana na beki wa Ethiopia, Tiruanchi Mengesh wakati wa mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Ethiopia ilishinda 1-0.
Mchuano wa wachezaji wa Tanzania na Ethiopia kwenye dimba la Uwanja wa Taifa, ulivyokuwa jijini leo jioni. wachezaji wakioneshana ufundi wa kuudhibiti mpira.
![]() |
| Mchezaji wa timu ya Twiga Stars Mawanahamisi Omary akiruka juu kuuwahi mpira uliokuwa ukiwaniwa pia na mchezaji wa Ethiopia. |
Kocha wa timu ya Soka ya Wanawake ya Tanzania 'Twiga Stars' akiwa na huzuni baada ya kufungwa bao 1-0 na Ethiopia na kutolewa katika mashindano ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mshambuliaji wa Twiga Stars, Mwanahamis Omari 'Gaucho' akimtoka beki wa Ethiopia, Berktawet Girma
Wachezaji wa Ethiopia wakifurahia ushindoi wa timu yao.







No comments:
Post a Comment